*************************
NA EMMANUEL MBATILO,
TIMU ya Senegal imefanikiwa kunyakua kombe la AFCON mara baada ya kuichapa Misri kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kutoka sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za mchezo huo.
Katika kipindi cha kwanza dakika ya 7 ya mchezo Senegal ilipata penati baada ya mchezaji wao Saliou Ciss kuchezewa rafu ndani ya boksi lakini penati hiyo iliyopigwa na Saidio Mane ilipanguliwa na kipa wa Misri Mohamed Abougal.
Mchezo huo ulikuwa fainali ya aina yake ambapo timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu hata hivyo mpaka mpira unaisha hakuna timu iliyopata bao licha ya kupatikana kwa nafasi nyingi.
Mchezaji wa Misri aliyekosa penati ni Mohamed Abdelmonem pamoja na Mohanad Lasheen wakati kwa upande wa Senegal aliyekosa penati ni Bouna Sarr.
Saisio Mane ndiye aliyekuwa shujaa mara baada ya kucheza penati ya mwisho na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi