Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega akitabasamu wakati Rais Samia Suluhu Hassan aliposimama Lamadi-Busega kuwasalimia wananchi.
……………………………………………………
Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Veronica Sayore kwa kusimamia vyema fadha za ujenzi wa madarasa 95 yaliyojengwa chini ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapamabno dhidi ya UVIKO-19.
Rais Samia amesema hayo akiongea na wananchi eneo la Lamadi Wilayani Busega tarehe 04/02/2022 akiwa njiani kuelekea mkoani Mara kwaajili ya ziara ya kikazi.
“Kituo nilichotoka nimetengua wakurugenzi wanne kutokana na ubadhilifu na matumizi mabaya ya fedha, kwako sijasikia, nimefurahi endelea kuchapa kazi Mkurugenzi, alisema Rais Samia.