Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akisalimiana na Viongozi wa Wanachama wa Chama hicho mara baada ya kuwasili katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 45 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika katika Uwanja wa Karume, Musoma Mkoani Mara.
Vijana wa halaiki wakionyesha michezo mbalimbali wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 45 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika katika Uwanja wa Karume, Musoma Mkoani Mara.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali, Wanachama wa Chama hicho pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Musoma katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 45 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika katika Uwanja wa Karume, Musoma Mkoani Mara.
Viongozi mbalimbali,Wananchama wa CCM pamoja na wananchi wakifatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 45 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika katika Uwanja wa Karume, Musoma Mkoani Mara
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Kadi yake namba 1 ya Kieletroniki ya Chama Cha Mapinduzi CCM kutoka kwa Katibu wa Chama hicho Ndugu Daniel Chongolo mara baada ya kuzindua Rasmi zoezi la ugawaji wa Kadi hizo katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 45 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika katika Uwanja wa Karume, Musoma Mkoani Mara.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kwenye Kompyuta kuzindua Rasmi Kadi za Kieletroniki za Chama cha Mapinduzi CCM katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 45 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika katika Uwanja wa Karume, Musoma Mkoani Mara.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa Kadi yake namba 1 ya Kieletroniki ya Chama Cha Mapinduzi CCM kutoka kwa Katibu wa Chama hicho Ndugu Daniel Chongolo mara baada ya kuzindua Rasmi zoezi la ugawaji wa Kadi hizo katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 45 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika katika Uwanja wa Karume, Musoma Mkoani Mara.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Kadi ya Kieletroniki Balozi wa CCM Paul Masinde kutoka Musoma Vijijini mara baada ya kuzindua zoezi hilo la Kadi.
……………………………………………………………………
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kadi mpya za wanachama za kielektroniki zenye taarifa na kumbukumbu muhimu za mwanachama zitakazowatambulisha na kuwawezesha kupata huduma za kifedha.
Uzinduzi wa kadi hizo umefanyika mjini Musoma leo Februari 5,2022 ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa chama hicho tawala kilichoundwa Februari 5, 1977 baada ya kuungana kwa vyama vya ukombozi vya Tanu (Tanganyika) na Afro Shirazi kwa upande wa Zanzibar.
Kadi hizo zimezinduliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia amekabidhiwa kadi ya kwanza na Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chongolo.
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amesema kupitia kadi hizo wanachama wa CCM zaidi ya 12 milioni siyo tu watatambulika kirahisi, bali pia wataweza kutumia kadi zao kupata huduma za kifedha.
Kwa mujibu wa Chongolo, wanachama zaidi ya 2.07 milioni tayari wamesajiliwa kupitia huo mfumo mpya wa kielektroniki.