…………………………………………….
Adeladius Makwega,DODOMA
Wakaazi kadhaa wa kata ya Ketaketa hawana mawasiliano kabisa na wenzako wa kata ya Ilonga na Mahenge Mjini kuelekea mkoani Moarogoro baada ya daraja kubwa linalounganisha kata hizi mbili kukatika baada ya mvua kubwa zinazonyesha katika eneo hilo.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hii njia ya simu, wakaazi hao wamesema kuwa daraja hilo lililojengwa awali tangu wakati wa utawala wa Mjerumani lilikuwa imara hadi mwaka 2018 ambao lilibomolewa na mvua kubwa zilizonyesha wakati huo na kukajengwa daraja shikizi la muda la ambalo lenyewe ndilo lililokuwa msaada kwao kwa miaka minne sasa na limebomoka kabisa na hakuna mawasiliano kwa sasa.
Wananchi wamesema kuwa serikali ilipojenga daraja la hilo la dharura ambalo nalo ndilo limebomoka Februali,1 2022 na kusababisha kero kubwa kwa wananchi wa kata hiyo ambayo ni mwisho kabisa katika wilaya ya Ulanga na mkoani Morogoro inayopakana na mkoa wa Lindi.
Akizungumzaa kwa niaba ya wananchi hao kwa njia ya simu baada ya kupata mtandao Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM wa kata ya Ketaketa ndugu Pankras Pankrasi Mtemike amesema kuwa kukatika kwa daraja hilo imekuwa kero ambayo imedhoofisha hata shughuli zingine za kijamii katani kwao.
“Hali ni mbaya, mathalani leo wanafunzi kadhaa wameshindwa kwenda shuleni kutokana na kushindwa kuvuka maji labda wale wakubwa waliweza kuweka magogo na kuuvuka mto Ikangao na kwenda masomoni, huku kipindi hiki mamba wakilandalanda katika mito hiyo.”
Kiongozi huyu amesema kuwa shule ambazo zimeathirika na kubomoka na daraja hilo ni shule ya msingi Ikangao na Shule ya Msingi na Sekondari Luhombero. Huku hata Wananchi wanaotakiwa kwenda kupata huduma za tiba Tarafani Mwaya kwenye kituo kikubwa cha Afya nao imekuwa vigumu labda hadi maji yakipungua ndipo watakapovuka mto huo wa Ikangao
Kiongozi huyu wa Umoja wa Vijana wa CCM alisema kuwa Kata ya Ketaketa inategenea mno uchumi wake katika kilimo cha mazao kadhaa ikiwamo ufuta, mpunga, ndizi na mazao mengine na kuyasafirisha kwenda masokoni Mahenge, Morogoro na Dar es Salam.
“Ninaomba serikali ijenge daraja la kudumu, hoja za kusema wakandarasi wanakuja kupima mchanga haina mashiko, wasiogope gharama wananchi Ketaketa tunahitaji daraja la kudumu na wala siyo lami.” Aliongeza Kiongozi huyo wa CCM.
Tangu mwaka 2018 sasa ni miaka mine hakuna malori makubwa yaliyokuwa yanaweza kuvuka kwenda Ketaketa kuuchukua mazao na kama daraja lingekuwepo njia hii inaweza kutokea hadi Lindi aliomba barabara hiyo kutengenezwa mapema.
Daraja hili lililobomoka linapita juu ya mto Ikangao ambao unakusanya maji yote yanayotokea Kitongoji cha Mrundu chenye mito mingi mikubwa na kuyamwaga katika Mto Ikangao na kuyapeleka katika Mto Mkubwa wa Luhombero.