Katibu Tawala msaidizi upande wa uchumi na uzalishaji Dkt Rozalia Lwegasila (wakati) Mkurugenzi wa ukuzaji viumbe maji kutoka wizara ya mifugo na uvuvi Dkt Nazael Amosi (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa ugani wa uvuvi wanaosimamia ukuzaji wa viumbe maji kutoka mkoa ya Kilimanjaro, Pwanai, Daer es salaam, Arusha, Tanga na Morogoro. Bwawa la kukuzia viumbe maji katika kituo cha Kingolwila mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa ukuzaji viumbe maji kutoka wizara ya mifugo na uvuvi Dkt Nazael Amos Madalla akitoa mafunzo kwa maafisa ugani wa uvuvi unaosimamia shughuli za ukuzaji viumbe maji katika kituo cha kituo cha Kingolwila mkoani Morogoro February 1,2022.
*************************
Na Farida Said
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bi Maliam Mtunguja amewataka watanzia kuchangamkia fulsa zilizopo katika uchumi wa bluu kutokana na kuwepo rasilimali maji ikiwemo bahari, maziwa, mito na maeneo oevu ambayo yanatoa wigo mpana wa kufanya shughuli za ufugaji wa samaki na viumbe wengine wa majini.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Katibu Tawala msaidizi upande wa uchumi na uzalishaji Dkt Rozalia Lwegasila wakati wa kufungua mafunzo rejea kwa maafisa ugani wa uvuvi kutoka mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha na Pwani, amesema wizara kupitia vituo vyake vya kuzalisha viumbe maji imezalisha vifaranga vya samaki 3,191,160 katika Mwaka 2021.
Amesema licha ya Serikali kuwekeza nguvu kubwa katika sekta ya mifugo na uvuvi, bado kuna uzalishaji mdogo wa mazao ya viumbe maji ukilinganisha na fulsa zilizopo nchini, hii inachagizwa na ukosefu wa elimu kwa wananchi inayosabaishwa na upungufu wa maafisa ugani wa uvuvi.
“Tasnia ya ukuzaji viumbe maji inakabiliwa na upungufu wa maafisa ugani 15,323 ambapo kwa sasa kuna maafisa ugani 677 ikilinganishwa na mahitaji ya maafisa ugani 16000.” Alisema Dkt Lwegasila.
Sambamba na hayo amewataka maafisa ugani kupeleka teknolojia walioipata kwa watanzania ili waweze kufuga samaki na viumbe maji wengine kisasa zaidi na kuendana na soko la dunia kwani kwa sasa kuna uhitaji mkubwa wa kitoweo cha samaki.
Amesema kutokana na ungezeko kubwa la watu hapa nchini pia mahitaji ya samaki yameongezeka maradufu ambapo ulaji wa samaki wa kilogramu 8.5 kwa mwaka haukidhi mahitaji na kuwataka watanzania kuwekeza katika ufugaji wa samaki.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkurugenzi wa ukuzaji viumbe maji kutoka wizara ya mifugo na uvuvi Dkt Nazael Amos Madalla amewahimiza watanzania kufuga samaki na viumbe maji wengine ili kujiongezea kipato chao na Taifa kwa ujumla.
Aidha amesema Wizara ya mifugo na uvuvi imejipanga katika kuhakikisha ufugaji wa samaki unakuwa na tija kwa kuanzisha vituo vya ukuzaji viumbe maji ambapo mpaka sasa kuna vituo 5 vinavyoweza kutoa elimu sahihi kuhusu ufugaji wa samaki pamoja na vifaranga.
Kwa upande wao maafisa ugani wameishukuru wizara ya mifugo na uvuvi kwa kuwapatia mafunzo ambayo yatakuwa chachu katika kukuza uzalishaji wa viumbe maji katika maeneo yao.