Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson akila kiapo cha uaminifu mbele ya Waheshimiwa Wabunge mara baada ya kuchaguliwa kwa kura zote 376 za Wabunge waliokuwa Bungeni kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waheshimiwa Wabunge wakimsindikiza Spika Mpya wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kuingia ukumbi kwa ajili ya kula kiapo cha uaminifu mara baada ya kuchaguliwa kwa kura zote 376 za Wabunge waliokuwa Bungeni. Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) katika picha ya pamoja na Maspika Wastaafu, Mhe. Anne Makinda (kushoto) na Pius Msekwa (kulia) mara baada ya kuapishwa Bungeni Jijini Dodoma. Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uongozi Jijini Dodoma.
PICHA NA BUNGE
************************
Na mwandishi wetu.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemchagua Dkt.Tulia Ackson (CCM) kuwa Spika wa bunge hilo kwa asilimia 100.
Jumla ya kura 376 zimepigwa na wabunge hao ambao ni sana na ASILIMIA 100 kura zote zikienda kwa Dkt Tulia Ackson.
Kiti cha USPIKA kilikuwa na wagombea tisa wagombea hao ni Abdullah Mohammed Said (NRA), Mhandisi Aivan Jackson Maganza (TLP), David Daud Mwaijojele (CCK), Georges Gabriel Bussungu (ADA -TEA), Kunje Ngombale Mwiru (SAU),
Wengine Maimuna Said Kassim (ADC), Ndonge Said Ndonge (AAFP), Saidoun Abrahamani Khatib (DP) na Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson.