******************************
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema kamwe Jeshi hilo alitavumilia vitendo vya kujichukulia sheria mkononi vinayofanywa na baadhi ya watu wa jamii ya wakulima na kifugaji ambapo katika wilaya ya Kilindi mkoani Tanga zaidi ya watu 20 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na mapigano ya wakulima na wafugaji yaliyotokea Januari 30 katika kata ya Kibirashi na Elerai na kusababisha vifo vya watu sita.
IGP Sirro ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya kutembelea wilaya ya Kilindi mkoani Tanga kwa lengo la kuzungumza na wananchi mbalimbali wa jamii za kifugaji na wakulima ambao wameathirika kutokana na mapigano yaliyohusisha jamii hizo mbili na kusababisha vifo pamoja na majeruhi.