KAMATI ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamempitisha Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson kuwa mgombea nafasi ya Spika wa Bunge kupitia chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika kesho Jumanne, Februari Mosi bungeni jijini Dodoma.
Shughuli ya upigaji kura iliendeshwa kwa wabunge kupiga kura za ndiyo na hapana baada ya ushauri uliotolewa na Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde kukubaliwa na wabunge.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge wa CCM, Kassim Majaliwa amesema idadi ya wabunge waliopiga kura walikuwa ni 340.