Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Lughano Kusiluka (kulia) akimkabidhi zawadi “Trophy” yenye ramani ya Tanzania na ramani ya chuo Kikuu Mzumbe, Prof.Percy Sepeng kiongozi wa ujumbe kutoka chuo kikuu cha “ Central University of Technology – CUT‘ kilichopo nchini Afrika Kusini
Kiongozi wa ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha “ Central University of Technology – CUT‘ kilichopo nchini Afrika Kusini, Prof.Percy Sepeng, akizungumza na Menejimenti ya chuo kikuu Mzumbe.
Dkt.Ntsoaki Malebo (kulia) na Bwn. Berbard Masoso kutoka Afrika kusini wakifuatilia majadiliano wakati na kikao na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe.
Wajumbe wa Afrika Kusini na Chuo kikuu Mzumbe, wakijadili kuhusu kuanzisha ushirikiano baina ya vyuo hivyo.
Ujumbe kutoka Afrika Kusini na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe, wakiwa katika picha ya pamoja.
Kiongozi wa ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha “ Central University of Technology – CUT‘ kilichopo nchini Afrika Kusini Prof. Percy Sepeng, akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili chuo kikuu Mzumbe, pembeni ni Dkt. Ntsoaki Malebo Mkurugenzi Mwandamizi wa kituo cha ubunifu na mafunzo wa chuo hicho.
……………………………………………………………
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, leo amepokea ujumbe wa wawakilishi kutoka Chuo kikuu cha “ Central University of Technology – CUT (Free State)‘ cha Afrika Kusini, waliotembelea makao makuu Morogoro kwa lengo la kuangalia fursa za ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika nyanja za kitaaluma na uendeshaji.
Akizungumza katika kikao cha utambulisho Prof.Kusiluka kwa niaba ya Menejimenti, amesema Chuo Kikuu Mzumbe kina fursa nyingi za ushirikiano hasa katika masuala ya ubovu katika ufundishaji ikiwemo Menejimenti na Utawala, Biashara na Ujasiriamali, Ubunifu na Teknolojia, Sheria, Mifumo ya Afya na Tathmini, Ununuzi na Ugavi, Sayansi na Teknolojia, Uhasibu na Usimamizi wa Fedha, Sayansi ya Jamii, Elimu na maeneo mengineno, na hivyo kukihakikishia chuo cha “CUT” fursa nyingi za ushirikiano kutokana ujuzi na uzoefu wa muda mrefu katika ufundishaji tangu chuo hicho kilipoanzishwa mwaka 1972.
Naye mwakilishi wa Chuo Kikuu cha CUT, Prof. Percy Sepeng, amesema, kwa ujumla wamefurahishwa na namna Chuo Kikuu Mzumbe kinavyoendeshwa na kutoa elimu katika maeneo mbalimbali ya ubobevu na kwamba wanategemea kujifunza mengi kutoka Mzumbe, kutokana na uzoefu waliouona katika ufundishaji hususani katika sekta ya Mifumo ya Afya, Utawala wa Umma, Menejimenti na Utawala n.k
Kikao hicho kimeazimia vyuo hivyo viwili kuanzisha ushirikiano katika maeneo mengi ya kitaaluma na hivyo wameona ni wakati muafaka kushirikiana na kuweza kuboresha mitaala itakayokuwa na maudhui yaliyotengenezwa kwa kuakisi mazingira halisi ya kiafrika ili kuweza kuwasaidia watu wa Kusini mwa Afrika katika changamoto za ajira na masuala mengine ya maendeleo.
Naye Afisa Uboreshaji wa Chuo hicho Bw. Bernard Matsoso amesema wamevutiwa na mfumo wa vyuo vya Umma nchini Tanzania kwa jinsi vilivyokuwa na utambulisho wake na kwamba wanatamani kujifunza zaidi “ tunatamani kujifunza kwenu jinsi mnavyoshughulika na wanafunzi wa makundi tofauti wakiwemo wenye ulemavu, tamaduni na dini tofauti na zaidi namna mlivyofanikiwa kufanya lugha ya Kiswahili kuwa ni lugha ya kufundwa vyuoni hususani katika kipindi hiki ambacho Kiswahili kimekuwa moja ya lugha kubwa inayotumika sehemu nyingi Barani Afrika” Alisema
Ushirikiano huo umelenga kuanza pamoja na mambo mengine, kuanzishwa kwa program za pamoja zitakazotoa matokeo bora na kuweza kuwasaidia zaidi vijana wa Kusini mwa Afrika, kutatua changamoto za ajira na matumizi ya teknolojia.