Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akikabidhi cheti cha kutambua mchango wa kampuni ya Vodacom katika kupunguza mgawanyiko wa kidijitali nchini kwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Sitholizwe Mdlalose wakati wa kongamano la Bridging the digital divide lilioandaliwa na Mwananchi Communication Ltd na kudhamiwa na Vodacom Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communication Ltd, Bakari Mwachumu.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (watano kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Vodacom, Sitholizwe Mdlalose (watatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communication Ltd , Bakari Mwachumu (wanne kulia), Mwenyekiti wa bodi MCL, Leonard Mususa (watano kushoto), na waendesha mada (Panelists) wakati wa kongamano la Bridging the digital divide lilioandaliwa na Mwananchi Communication Ltd na kudhamiwa na Vodacom Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose akizungumza na hadhira kwenye kongamano la Bridging the digital divide lililofanyika jijini Dar es Salaam