Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi , Mhandisi Zena Ahmed Said,akimkabidhi Begi la Skuli, Fomu na Vifaa vyengine Mtoto Zahor, ,(Kulia ) ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taqwa Dkt. Salha Mohammed Kassim, hafla ya Ugawaji wa Vifaa vya Skuli kwa Watoto Yatima, imefanyiaka Ukumbi wa Skuli ya Nasari Saateni Mjini Zanzibar.
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi , Mhandisi Zena Ahmed Said, akipiga Picha na Mtoto Nassra baada ya kumkabidhi Begi lenye Vifaa vya Skuli ndani yake,(Kulia ) ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taqwa Dkt. Salha Mohammed Kassim, katika hafla ya Ugawaji wa Vifaa vya Skuli kwa Watoto Yatima, huko Ukumbi wa Skuli ya Nasari Saateni Mjini Zanzibar.
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi , Mhandisi Zena Ahmed Said (kulia), akikabidhi fedha shilingi milioni Moja , kwa niaba ya Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Sharifa Omar Khalfan, kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taqwa Dkt. Salha Mohammed Kassim, kwa kuichangia Taasisi hiyo. katika hafla ya Ugawaji wa Vifaa vya Skuli kwa Watoto Yatima, huko Ukumbi wa Skuli ya Nasari Saateni Mjini Zanzibar. Baadhi ya Watoto na Wazazi waliyohudhuria katika hafla ya Ugawaji wa Vifaa vya Skuli kwa Watoto Yatima, huko Ukumbi wa Skuli ya Nasari Saateni Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taqwa Dkt. Salha Mohammed Kassim akitoa maelezo kuhusu Taasisi hiyo, katika hafla ya Ugawaji wa Vifaa vya Skuli kwa Watoto Yatima, huko Ukumbi wa Skuli ya Nasari Saateni Mjini Zanzibar.
(PICHA NA MARYAM KIDIKO – HABARI MAELEZO.)
**************************
Na Khadija Khamis –Maelezo 30/01/2022,
Taasisi ya TAQWA Orphans Trust Tanzania,imetoa msaada wa vifaa vya Shule vyenye thamani ya zaidi milioni 25 za Kitanzania kwa ajili ya watoto yatima wa Zanzibar,
Akitoa Msaada huwo Katibu Mkuu Kiongozi ,Mhandisi, Zena A.Said katika Skuli ya Maandalizi Saateni alisema mchango huo umetolewa na wafadhili mbali mbali ambao wamejaaliwa kutoa ikiwemo sare za shule ,viatu, mkoba, mabuku pamoja na kalamu.
Amesema kuchangia yatima hakuchagui mwanamke au mwanamme ,muislamu na asiye muislamu Yule ambaye anataka kupata heri anakaribishwa kupeleka kwenye taasisi hiyo ili watoto hao wapate furaja,
“Siyo lazima mtu kuwa tajiri ndio achangie hata masikini kwa uwezo ulionao unaweza kusaidia kulingana na hali yake hakuna kutoa kudogo mbele ya Mwenyezi Mungu”alisema Katibu Mkuu .
Amesema mtoto akipelekwa kituo cha kulelea watoto yatima na ikawa familia ikashindwa kumlea humpa unyonge mkubwa na kumkosesha mapenzi kwa familiya yake
Amesema Taqwa inawashughulikia watoto yatima ambao wanalelewa na mzazi au mlezi ambae hana uwezo wa kumpatia huduma zote za msingi,
ya TAQWA Orphans Trust Tanzania Salma Mohamed Kassim amesema taasisi hiyo huwasaidia wazazi na walezi kimapato kwa kuwapatia huduma mbali mbali ikiwemo vifaa vya shule ,huduma za afya pamoja na msaada wa vyakula ,
Amefahamisha kuwa lengo la taasisi hiyo ni kuwapa furaha watoto yatima wanaolelewa majumbani mwao Tanzania kwa kuwasaidia kupata mahitaji yao ya msingi na ya kijamii
Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa jamii kujiunga katika taasisi hiyo ili kuzidishi nguvu na uimara wa kuendeleza juhudi hizo ,
.Amesema Taasisi ya Taqwa imeweza kupata mafanikio zaidi ya miaka 12 kwa mpande wa Tanzania na Zanzibar ina watoto 478 ambao wanapata msaada katika Taasisi hiyo
Hata hivyo taasisi hiyo imeeleza changamato mbali mbali ikiwemo ukosefu wa thamani ya ofisi pamoja na usafiri kwa ajili ya ufuatiliaji wa huduma.