Msajili wa Hazina Bw.Mgonya Benedicto,akizungumza wakati akifunga Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) uliofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Bw.Elisa Mbise,akiwapongeza washiriki kwa kushiriki Mkutano huo wakati wa kufungwa kwa Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) uliofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrice Mbodo,akizungumzia waliojifunza katika Mkutano huo wakati wa kufungwa kwa Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) uliofanyika jijini Dodoma.
Washiriki wakifatilia hotuba ya Msajili wa Hazina Bw.Mgonya Benedicto (hayupo pichani) wakati akifunga Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) uliofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrice Mbodo,akiteta jambo na Msajili wa Hazina Bw.Mgonya Benedicto wakati wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) uliofanyika jijini Dodoma.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi Shirika la Posta Tanzania Bi.Halima Abdallah Hamad,akitoa neno la shukrani kwa Msajili wa Hazina Bw.Mgonya Benedicto (hayupo pichani) mara baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) uliofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrice Mbodo akikabidhi zawadi ya kalenda na shajara (Diary) kwa Msajili wa Hazina Bw.Mgonya Benedicto mara baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) uliofanyika jijini Dodoma.
Msajili wa Hazina Bw.Mgonya Benedicto (katikati waliokaa) akiwa katika picha pamoja na washiriki mara baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) uliofanyika jijini Dodoma.
…………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,DODOMA
MSAJILI wa Hazina, Mgonya Benedicto amelitaka Shirika la Posta Tanzania kutumia kwa weledi fedha zilizotolewa na serikali ili kukidhi matarajio yake.
Aidha, ameagiza kuwepo na ubunifu katika kutekeleza majukumu ya Shirika kisheria ili kuongeza mapato na kutoa gawio stahiki katika Mfuko Mkuu wa Serikali.
Hayo ameyasema wakati akifunga Mkutano wa 28 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika hilo uliofanyika jijini Dodoma.
Amebainisha kuwa Mwaka jana serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iliamua kuchukua jukumu la kuwalipa wastaafu wa liliyokuwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki na kurejesha kiasi chote cha Sh.Bilioni 7.9 ambacho kilikuwa hakijarejeshwa.
“Serikali ilifanya maamuzi haya ili kuweka mazingira wezeshi kwa shirika kuongeza uzalishaji na kutekeleza majukumu yake ili kuendana na lengo la uanzishaji wa shirika na kwa mujibu wa sheria iliyounda shirika…Kwa kuwa serikali ilifanya maamuzi haya ili kuongeza uzalishaji na kujipambanua katika utendaji wake napenda kuwasihi na kuelekeza kutumia fedha hizo kwa weledi ili kutimiza azma hiyo ya serikali na muende mbali zaidi ya mategemeo,”amesema.
Msajili huyo amesema Ofisi yake itaendelea kushirikiana na Shirika katika utatuzi wa kero za kiuendeshaji na kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa kushirikiana na serikali ikiwamo suala la mtaji wa shirika na malimbikizo ya madeni ya kodi ya muda mrefu ya Sh.Bilioni 26.
Awali, Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Macrice Mbodo, alisema wajumbe wa baraza hilo wamepatiwa mafunzo mbalimbali ikiwamo ya kujengewa uwezo wa kiuongozi bila kusukumana wala kusigana huku akishukuru jitihada za Ofisi ya Hazina kubeba mzigo wa kulipa malimbikizo ya madeni ili shirika liweze kukopesheka.
Amesema shirika linatambua kuna jitihada zinafanywa na ofisi hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha ili kuliwezesha Shirika ambalo halijawahi kupewa mtaji tangu kuanzishwa kwake licha ya kuwa Sheria ilitaka Shirika hilo lipewe mtaji wa uendeshaji.
“Lipo andiko ambalo tumeliandika kwa kushirikiana na Ofisi yako, Wizara yetu ambalo lipo Wizara ya Fedha na Ofisi yako inaendelea kufuatilia tunaamini chini ya ofisi yako na jitihada zinazoendelea ipo siku shirika litapata fedha hizi,”amesema.