Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro N. Kilahala katikati akizungumza na wakurugenzi, mameneja na wakuu wa vitengo wa Wakala huo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha mapitio ya utendaji kazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme kwa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 pamoja na maandalizi ya maoteo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ufundi VETA Mkoani Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Matengenezo Mhandisi Alex Rumanyika na kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji Bi. Monica Moshi.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Bi. Monica Moshi akizungumza na wakurugenzi, mameneja na wakuu wa vitengo wa Wakala huo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha mapitio ya utendaji kazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme kwa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 pamoja na maandalizi ya maoteo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ufundi VETA Mkoani Dodoma. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro N. Kilahala na kushoto ni Meneja wa Mipango Senzo Gwanchele.
Mkuu wa Karakana ya Wilaya ya Same Mhandisi David Katua akichangia jambo wakati wa kikao cha mapitio ya utendaji kazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme kwa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 pamoja na maandalizi ya maoteo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ufundi VETA Mkoani Dodoma.
Wakurugenzi, mameneja na wakuu wa vitengo kutoka vituo mbalimbali vya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Lazaro N. Kilahala (hayupo pichani) wa kikao cha mapitio ya utendaji kazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme kwa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 pamoja na maandalizi ya maoteo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ufundi VETA Mkoani Dodoma.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO
………………………………………………
Na. Alfred Mgweno (TEMESA Dodoma)
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro N. Kilahala amewaagiza mameneja na wakuu wa vituo vya Wakala huo kuhakikisha wanakuwa na mipango sahihi ya kitaasisi ambayo itawezesha TEMESA kuwa na mafanikio kwa kupanga mipango sahihi na kwa wakati huku wakihakikisha inatekelezeka na inaleta tija ambayo imekusidiwa.
Mtendaji Mkuu ameyasema hayo mapema leo wakati akizunguma na mameneja wa vituo, wakuu wa idara na wakurugenzi wa Wakala huo katika kikao cha mapitio ya utendaji kazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme kwa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 pamoja na maandalizi ya maoteo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ufundi VETA Mkoani Dodoma.
Ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto kubwa zinazoukabili Wakala ni uzalishaji na ukusanyaji ambapo unaanzia nyuma katika utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka zinazohitajika ili kuweza kufanikisha ukusanyaji wa madeni ya nyuma. Mtendaji Mkuu amesema kuwa kitu kitakachofanyika tofauti ni kufanya maoteo ya ukusanyaji wa madeni ya nyuma na kile ambacho kituo kimepanga kukusanya kwa mwaka husika.
Aidha aliongeza kuwa ameanzisha utaratibu tofauti wa kupima uzalishaji wa kila Mkoa ambapo kwa sasa Mameneja watapimwa kwa uzalishaji, ukusanyaji wa madeni na ukusanyaji wa kazi ambazo wamezalisha kwa wakati husika.
‘’Tutatengeneza makubaliano ya kiutendaji ambayo yatakuwa ni baina ya kila meneja na msimamizi wa kituo ambapo atasaini na Mtendaji Mkuu, katika vitu tutakavyoviweka kama vipimio itakuwa sio tu uzalishaji bali kutakuwa pia na ukusanyaji wa deni la nyuma na ukusanyaji wa kazi iliyozalishwa.’’ Amesema Mtendaji Mkuu.
Mtendaji Mkuu pia amefanya mabadiliko madogo kwa upande wa vivuko ambapo kuanzia sasa kutakuwa na meneja wa vivuko wa kanda ambapo kutakuwa na kanda mbili, kanda moja ya Ziwa ambapo meneja atakuwa na jukumu la kusimamia vivuko vyote vya mikoa iliyopo kanda ya Ziwa huku kituo chake kikiwa ni Mkoani Mwanza. Aidha kutakuwa na meneja wa vivuko kanda ya Mashariki na Kusini ambaye atasimamia vivuko vyote vya kanda hiyo na wakuu wote wa vivuko watakuwa wakiripoti kwa mameneja hao wa kanda.
Hatua hiyo itawasaidia mameneja wa karakana za mikoa kwa kuwapunguzia mrundikano wa majukumu na sasa watakuwa wakisimamia tu shughuli za karakana na kuachia majukumu ya vivuko kwa meneja wa kanda husika.
Naye Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Bi Monica Moshi akizungumza katika kikao hicho amewaomba mameneja hao kuanza kwenda na kasi ya Mtendaji Mkuu kwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidi na kuleta tija kwa Wakala
‘’Wote sisi tunaendesha gari moja ninaamini kwamba tutaweza kuendesha gari letu liende mbele’’, alisema Mkurugenzi na kumshukuru Mtendaji Mkuu kwa mawazo mapya ambayo ameyaleta na mabadiliko katika TEMESA.
Kikao hicho cha utendaji kazi kinatarajiwa kuchukua siku tatu ambapo kuanzia siku ya kesho mameneja hao wataungana na wahasibu kwa ajili ya uundaji wa mipango ya bajeti za mikoa za mpango wa muda wa kati na mrefu (MTEF) ikiwa ni pamoja na kuingiza mpango huo kwenye mfumo wa kibajeti (PLANREP).