*****************
Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Wizara yake kupitia Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) itaanza kugawa mirahaba kwa kazi mbalimbali za wasanii zinazotumika kwenye redio kila baada ya miezi sita ili waweze kunufaika na kazi zao.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa utoaji wa tuzo za muziki na ugawaji wa mirahaba kwa wasanii Januari 28, 2022 kwenye Ukumbi wa kimataifa cha Julius Nyerere. Mhe Mchengerwa amesema Wizara yake inakwenda kufanya mapinduzi makubwa kwenye sekta hizo katika kipindi kifupi kijacho ambapo amewataka watendaji wa Serikali kufanya kazi kwa kasi na weledi.
Ametoa muda wa wiki tatu kwa watendaji wa Wizara kuandaa App maalum itakayoitwa “sema na Waziri wa Utamaduni “ ambayo itatoa fursa kwa wadau mbalimbali wa sekta ya Sanaa, utamaduni na Michezo kuwasiliana moja kwa moja na yeye pindi wanapotaka kuwasiliana naye badala ya mfumo wa sasa uliozoeleka.
“Naomba niwaahidi hapa kuwa nitakuwa nanyi na milango itakuwa wazi wakati wowote ili kila mmoja wenu mwenye shida aweze kusaidiwa kikamilifu, hii Wizarani kwa ajili yenu inapaswa mfaidike nayo” amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Amelielekeza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuhakikisha kuwa linafanya kazi yake ya kukuza, kuendeleza na kuwasaidia wasani wa Tanzania kwa weredi na waache mara moja kufanya kazi kwa mazoea, ambapo amesisitiza kuwa waanzekupanga kwa ajili ya kuandaa tuzo kubwa za kimataifa.
Akizungumzia mchakato wa utoaji wa Tuzo za Muziki ambazo kilele chake kitakuwa Machi 26, 2022 amelitaka BASATA kuhakikisha linatenda haki ya ili kupata kazi zenye kiwango bora.
“Natambua huko nyuma kumekuwa na malalamiko naomba niwaonye, mimim katika kipindi change hakutakuwa na tuzo za msongo”: amesisitiza Mhe Mchengerwa.
Amewashauri wasanii wawe na mazoea ya kujisajiri COSOTA ili kazi zao ziweze kutambulika na waweze kunufaika na kazi hizo.Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Pauline Gekul amesema Sekta za utamaduni, Sanaa na michezo zina umuhimu mkubwa kwa taifa ndiyo maana kiutokana na umuhimu huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Sulkuhu Hassan aliamua kuziundia Wizara hiyo huku akitoa sekta ya habari.
Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikakli imefufua tuzo za muziki baada ya miaka saba kutokuwepo hivyo wadau wa sanaa kwa kushirikiana na Serikali wana wajibu wa kuzilinda na kuzienzi ili ziendelee kuwanufaisha.
Naibu Katibu Mkuu, Saidi Yakubu amesema sekta ya Sanaa inagusa maisha ya wananchi wote wa Tanzania kwa namna moja au nyingine hivyo Wizara itahakikisha inaandaa mazingira bora ili wasanii waweze kunufaika na kuboresha maisha yao.
Katika tukio hilo Mhe. Mchengerwa amewaongoza mamia ya wadau waliohudhuria hafla hiyo kuimba wimbo wa hongera mwanangu wa Bibi Titi Mohamed huku akifafanua kwamba toka enzi za ukoloni muziki ulitumika katika ukombozi wa Tanzania.