Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Viongozi na Watumishi Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zilizopo chini ya Ofisi yake Jijini Dar es Salaam, Januari 27, 2022.
Sehemu ya Watumishi wa Kitengo cha Huduma za Ajira (TAESA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani).
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi akieleza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alipokutana na kuzungumza Viongozi na Watumishi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) hii leo Januiari 27, 2022
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Masha Mshomba akieleza jambo wakati wa mkutano huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akikabidhiwa Sheria na Miongozo ya Shirika hilo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa NSSF, Balozi Ali Siwa (katikati). Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Masha Mshomba.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi (kulia) akikabidhiwa Sheria na Miongozo ya Shirika hilo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa NSSF, Balozi Ali Siwa (katikati). Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Masha Mshomba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akipata taarifa kutoka kwa Afisa Huduma kwa Wateja Bi. Rehema Urembo (kushoto) alipotembelea ofisi hiyo Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya alipokuwa akikagua utekelezaji wa majukumu ya idara na vitengo katika Ofisi hiyo. Katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi.
**********************
Na: Mwandishi Wetu – Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amelitaka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuendelea kutoa kipaumbele kwenye sekta binafsi na sekta isiyo rasmi kwa lengo la kukuza sekta hizo.
Waziri Ndalichako ameeleza hayo wakati wa ziara yake ya Kikazi alipotembelea Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Januiari 27, 2022 Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu kwa kukagua utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zilizopo chini ya Ofisi yake.
Akizungumza mara baada ya kuwasili katika Makuu Makuu ya Ofisi hiyo alieleza kuwa, Sekta binafsi na sekta isiyo rasmi ni muhimu na zinaendelea kukua kwa kasi kutokana na sehemu kubwa ya wananchi kushiriki katika sekta hizo, hivyo ni vyema mfuko huo ukaandaa mazingira mazuri kwa wafanyakazi waliopo katika sekta hizo.
“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameendelea kuonyesha dhamira yake ya dhati ya kuweka mazingira bora kwa ajili ya wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na pia wafanyabiashara, mtumie fursa hiyo kuchangamkia sekta hiyo ili muendelee kutoa huduma ya hifadhii ya jamii katika maeneo hayo,” alieleza
“Mmeshuhudia hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya kikao na wafanyabiashara wadogo hapa nchini maarufu kama Machinga na aliahidi kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya biashara zao na kuwawezesha kiuchumi, hivyo mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii ni vyema ukahakikisha wafanyabiashara wadogo, mama lishe, bodaboda wanajiunga na kuwa wanachama wa mfuko huu,” alisema
Aliongeza kuwa, kutokana na mabadiliko ya Sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo yalifanyika mwaka 2018 kwa lengo la kutoa huduma ya hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi wa sekta hizo ni bora wananchi wakaendelea kupatiwa elimu ili kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa kujiwekea akiba katika sekta ya hifadhi ya jamii.
Aidha, Waziri Ndalichako alitumia fursa hiyo kuhimiza ushirikiano na umoja ili kufikia malengo ya utekelezaji wa majuku yao katika kuwatumikia wananchi.
“Nipongeze Uongozi na Watumishi kwa ujumla wa NSSF kwa kazi nzuri ikiwa ni pamoja na mnavyoendelea na jitihada za kuongeza wanacham wa mfuko,” alisema Waziri Ndalichako
Pia, Mheshimiwa Ndalichako aliwataka wanachama wa mfuko huo kutumia huduma ya NSSF KIGANJANI ambayo imekuwa ni mfumo mzuri wa kushughulikia huduma mbalimbali zinazohitajika kwa wanachama na kupunguza malalamiko ya wateja wa mfuko huo.
Kwa Upande Wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi alipongeza mfuko huo na kutaka watumishi katika shirika hilo kuendelea kutoa huduma bora za hifadhi ya jamii. Pia aliwataka watumishi hao kuwa wabunifu na wenye ari ya kutoa uelewa kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa NSSF, Balozi Ali Siwa alisema kuwa Shirika hilo linaendelea kukua hivyo Bodi hiyo itahakikisha inafanyakazi yake ya usimamizi ili malengo ya mfuko huo yaweze kufikiwa kwa ufanisi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Masha Mshomba aliahidi maagizo yote yaliyotolewa yatafanyiwa kazi kwa lengo la kuhakikisha mfuko huo unaendelea kutoa huduma za kuaminika na endelevu za sekta ya hifadhi ya jamii.