Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalum Dkt. Gwajima akizungumza na waomboleaji wakati wa msiba wa kijana Egidi Gangata, aliyefariki dunia kwa kuchomwa kisu jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalum Dkt. Gwajima,akisisitiza jambo kwa waomboleaji wakati wa msiba wa kijana Egidi Gangata, aliyefariki dunia kwa kuchomwa kisu jijini Dodoma.
Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalum,Tullo Masanja,akizungumza wakati wa msiba wa kijana Egidi Gangata, aliyefariki dunia kwa kuchomwa kisu jijini Dodoma.
Mwanafamilia Koku Selemani akisoma wasifu wa marehemu wakati wa msiba wa kijana Egidi Gangata, aliyefariki dunia kwa kuchomwa kisu jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bi.Rebeca Ndaki,akizungumza na waomboleaji wakati wa msiba wa kijana Egidi Gangata, aliyefariki dunia kwa kuchomwa kisu jijini Dodoma.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma Pelisiana Mboya,akizungumza na waomboleaji wakati wa msiba wa kijana Egidi Gangata, aliyefariki dunia kwa kuchomwa kisu jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalum Dkt. Gwajima akitoa heshima za mwisho kwa kijana Egidi Gangata, aliyefariki dunia kwa kuchomwa kisu jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalum Dkt. Gwajima,akiwaongoza waomboleaji kuelekea makaburini kwa ajili ya shughuli ya maziko ya kijana Egidi Gangata, aliyefariki dunia kwa kuchomwa kisu jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalum Dkt. Gwajima akiweka shada wakati wa msiba wa kijana Egidi Gangata, aliyefariki dunia kwa kuchomwa na kisu jijini Dodoma.
……………………………………………………………
Na Alex Sonna, Dodoma
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk.Dorothy Gwajima, ameshiriki maziko ya Egidi Gangata aliyefariki juzi kwa kuchomwa kisu maeneo ya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Kijana huyo ambaye ni miongoni mwa watoto wa mitaani aliuwawa na mwenzake walipokuwa wakigombea gundi.
Akizungumza kwenye maziko hayo leo, Dk.Gwajima ameeleza kuwa yeye na timu ya wataalamu kutoka Wizara yake, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma wamepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo hiki.
“Mimi na timu ya wataalamu wa serikali tulimfahamu mtuhumiwa tarehe 17/01/2022 tukiwa kazini kufuatilia na kujifunza juu ya changamoto za watoto waishio kwenye mazingira hatarishi eneo la Nyerere Square Jijini Dodoma ambapo, tulipofika tuliwakuta watoto na vijana kadhaa wa rika mbalimbali na katika kujitambulisha alikuwepo mtuhumiwa,”amesema
Aidha, amesema waliwaeleza vijana hao kuwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kubadilisha maisha ya watoto na vijana waishio mazingira hatarishi na kwa dhamira hiyo kwa kuundwa kwa Wizara hiyo mpya.
“Lengo la ziara ilikuwa ni kujifunza jinsi gani tuwasaidie kundi la watoto waishio mazingira hatarishi. Baada ya mazungumzo hayo tuliweza kuwashawishi vijana na watoto 13 akiwemo mtuhumiwa hivyo tukawapeleka Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo kwa ajili ya uchambuzi zaidi wa taarifa zao tuone jinsi ya kuwasaidia,”amesema
Amefafanua kuwa katika uchambuzi wa historia zao wataalamu walibaini baadhi ya vijana walishavuka miaka 18 akiwemo mtuhumiwa hivyo walikuwa hawaangukii kwenye sheria ya watoto chini ya kamishna wa ustawi wa jamii.
Aidha, amesema “Tulibaini kuwa wengi wao walikuwa tayari wameathirika na dawa za kulevya jambo lililohitaji wapate huduma ya afya kwanza. Hivyo, wizara iliwakabidhi vijana wa zaidi ya miaka 18 kwa wataalamu wa halmashauri ya jiji la Dodoma wanaohusika na Vijana kwa utaratibu zaidi ikiwemo huduma za afya.”
“Wakiwa kwenye uangalizi wa Jiji la Dodoma baadhi walitoroka akiwemo mtuhumiwa ambapo matokeo yake ameenda kusababisha mauaji. Kati ya wale 13 hadi sasa wako watoto sita wamebaki kwenye huduma na ustawi wa jamii na zoezi la kuwafikia na kuwanusuru watoto wa mitaani linaendelea mikoa yote hatua kwa hatua,”amesema.
Amesema tukio hilo la kusikitisha linatufundisha kuwa ndoto za watoto wengi zinapotea na tangu wakiwa watoto kwa kujikuta wameingia kwenye mkondo hasi wa mfumo wa maisha hususan maisha ya mitaani.
“Tunajua kuwa wako watoto wengine ambao wamekimbia nyumbani kwa sababu zilizo juu ya uwezo wao mfano kudhulumiwa, kuonewa, yatima wasio na msaada na waliowafanyiwa hivyo tutawasaka hadi tuwapate sheria ichukue mkondo wake,”amesema
Hata hivyo, amesema watoto wengine wako mtaani kwa sababu za kujitakia tu wakiamini kwenye maisha ya haraka haraka.
Kufuatia hali hiyo, Dk.Gwajima ametoa wito kwa viongozi ngazi mbalimbali kujipanga upya kutekeleza Mpango Kazi wa Kupambana na Ukatili wa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kwa kasi kubwa zaidi kwa ushirikiano na wadau wote waliopo ngazi husika na wajielekeze kupambana na mifumo inayosababisha kujitokeza kwa ukatili ikiwamo unaopelekea watoto kuishi mitaani.
“Pia natoa wito kwa wadau wote wa maendeleo ikiwemo asasi za kiraia, kidini, sekta binafsi, watafiti, wadau wa maendeleo na jamii kuungana na serikali kutafuta suluhu ya kudumu inayoendana na mazingira yetu na rasilimali zetu na ubunifu wetu,”amesema.