**************************
Na John Walter-Magugu,Babati.
Kuelekea sherehe ya maadhimisho ya miaka 45 tangu kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa February 5, jumuiya ya wazazi Mkoa wa Manyara, wametembelea shule ya sekondari Matufa, iliyopo Kijiji cha Magugu, nakupanda Miche ya miti , itakayowasaidia wanafunzi kujipatia vivuli.
Wakikabidhi miti hiyo katika shule ya sekondari Matufa, Leo January 26, Jumuiya ya wazazi CCM Mkoa wa Manyara, wameonyesha namna ambavyo wanajali nakutambua umuhimu wa kuwa na miti ya vivuli shuleni hapo, ikiwa ni Mara yao ya pili kutembelea shule hiyo nakupanda miche ya miti ambapo wamesifu jitihada za shule hiyo katika utunzaji wa miti kwani miti waliyoipanda hapo awali bado ipo.
Akizungumza na kituo hiki mkuu wa shule ya Matufa Sekondari, Hlen Anthony, amesema watahakikisha miti yote iliyoletwa shuleni hapo inakua vizuri, kwa kuimwagilia pamoja nakumpa kila mwanafunzi mti wake ili kuhakikisha miti yote inastawi.
Pia ameushukuru uongozi wa Jumuiya ya wazazi (CCM) Wilaya ya Babati VIJIJINI kwa kuendelea kupeleka miti shuleni hapo ikiwa ni Mara ya pili wanapeleka miti.
Kwaupande wa wanafunzi wa shule ya sekondari Matufa, wametoa shukuran zao kwa umoja huo wa wazazi, kuwapelekea Miche ya miti hiyo, kwani itawasaidia kujipatia hewa safi, vivuli pamoja na sehemu za kujisomea, na wameahidi kuitunza miti hiyo kwani ni muhimu kwao.
Mwenyekiti wa umoja wa wazazi Wilaya ya Babati Vijijini, Bw. Lumumba John Arra,Amesema kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 45 ya CCM, shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo kupanda miti, kutembelea makundi maalum pamoja na kutoa misaada mbalimbali.
Akikagua hatua za awali za ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Magugu, Lumumba amesema ni kata chache ambazo hazina ofisi za chama , hivyo ameipongeza Juimuiya wa wazazi Kijiji cha Magugu kwa kuanzisha ujenzi wa ofisi katika kata ya Magugu na kuwataka waanzishe harambeee (changizo) kwaajili yakupata fedha zitakazowawezesha kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo.
Kadhalika, Jumuiya ya wazazi imeandaa michezo mbalimbali ikiwemo mashindano ya kuendesha baiskeli, kukimbiza kuku, pamoja na kucheza bao kwa lengo la kutoa motisha kwa vijana wa Kijiji hicho.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Manyara Fratern Kwahhison, Maadhimisho hayo ya miaka 45 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi yanatarajiwa kufanyika tarehe 5 February 2022 tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 5/2/1977, ambapo kimkoa yatazinduliwa rasmi tarehe 29/1/2022 Sunya Wilayani Kiteto, na kilele itakuwa tarehe 5/2/2022 Wilaya ya Babati Mjini.