Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akionyeshwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzanite Forever Lapidary, Faisal Juma Shabhai, madini ya Tanzanite ambayo yamechongwa na kampuni hiyo iliyopo kwenye jengo la Soko la madini, Mererani wilayani Simanjoro, Januari 26, 2022. Alikuwa katika ziara ya kikazi ya mkoa Manyara. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishudia uchongaji wa madini ya Tanzanite uliokuwa ukifanywa na mtalaam, Jackline Saibulu wakati alipotembelea Kampuni ya Tanzanite Forever Lapidary iliyopo kwenye jengo la Soko la Madini, Mererani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, Januari 26, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kazi ya kuchonga madini ya Tanzanite wakati alipotembelea Kampuni ya Tanzanite Forever Lapidary iliyopo kwenye jengo la Soko la Madini, Mererani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, Januari 26, 2022. Watalaamu hao wa kuchonga madini ni Jackline Saibulu (kushoto) na Dorcas Steven. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama Tanzanite iliyochongwa wakati alipotembelea Kampuni ya Tanzanite Forever Lapidary iliyopo kwenye jengo la Soko la Madini, Mererani wilayani Simanjiro Januari 26, 2022. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Faisal Juma Shahbhai. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amevaa miwani maalum wakati alipokagua ubora wa madini ya Tanzanite katika kampuni ya Tanzanite Forever Lapidary iliyopo kwenye jengo la Soko la Madini, Mererani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, Januari 26, 2022. Alikuwa katika ziara ya kikazi ya mkoa huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Faisal Juma Shahbhai. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)