Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto mwenye kofia) na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania , Wiebe De Boer (katikati) wakisoma maandishi baada ya kuzindua Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi Manispaa ya Shinyanga
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi uliojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV – Netherlands Development Organization) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi umezinduliwa rasmi.
Uzinduzi huo umefanywa leo Jumatano Januari 26, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania , Wiebe De Boer katika eneo la Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania , Wiebe De Boer amesema mradi huo uliojengwa kwa gharama ya takribani Shilingi Milioni 310 una manufaa mengi ikiwemo kuimarisha usafi wa mazingira,kutokomeza magonjwa ya mlipuko na kusaidia kuzalisha nishati mbadala na mbolea kwa ajili ya kilimo.
Amesema mradi huo ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2017 utasaidia kuboresha upatikanaji na utumiaji wa huduma za usafi wa mazingira na kuboresha tabia ya usafi.
Boer ameushukuru na kuwapongeza wadau mbalimbali ukiwemo uongozi wa Manispaa ya Shinyanga na SHUWASA kwa kuupokea mradi na kuwapa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha kukamilika kwa mradi huo huku akiomba kuutunza na kuuendeleza uwe na manufaa zaidi kwa jamii.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ameishukuru Serikali ya Uholanzi kwa kuleta mradi huo mkoani Shinyanga huku akiahidi kuwa serikali ya mkoa wa Shinyanga ipo tayari kupokea miradi mingine kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
“Tanzania tumekuwa na urafiki na serikali ya Uholanzi,tunawashukuru kwa kutuletea mradi huu.Naomba tuulinde na kuuendeleza mradi huu uwe mkubwa kwani una manufaa makubwa kwa wananchi”,amesema Mjema.
“Maji taka ni dhahabu, maji taka ni mali tuliyoikalia kwani yanatumika kutengeneza mbolea kwa ajili ya kilimo na hata kuoteshea miti, mkaa na nishati mbadala”,amesema.
Mkuu huyo wa Mkoa ametumia fursa hiyo kuiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kutengeneza miundo mbinu ya kuzoa majitaka ili kuwezesha magari kuzoa majitaka na kuyapeleka kwenye mtambo huo wa kuchakata tope kinyesi.
“Tuendelee kutoa elimu kwa vijana watumie mbolea inayotokana na majitaka kwenye kilimo na hata kuoteshea miti. Wananchi sasa waamini kuwa majitaka ni mali na teknolojia hii mbadala ina manufaa na itasaidia kujiajiri ili kujiinua kiuchumi. Wananchi waamini kuwa majitaka yanaweza kutukwamua kiuchumi”,ameongeza Mjema.
Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA, Bi. Mwamvua Jilumbi amesema mradi huo utasaidia kuondokana na tabia ya umwagaji maji hovyo hivyo kutokomeza magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu na homa ya matumbo.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko amesema mradi huo utasaidia kutunza mazingira ya Manispaa ya Shinyanga huku akiomba wadau kuendelea kuleta miradi katika Manispaa hiyo.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto) na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania , Wiebe De Boer (katikati) wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi uliojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV – Netherlands Development Organization) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi leo Jumatano Januari 26,2022 katika eneo la Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) Kizumbi Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto) na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania , Wiebe De Boer (katikati) wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto) na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania , Wiebe De Boer jinsi Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania , Wiebe De Boer (katikati) akielezea kuhusu Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Mkuu wa Idara ya Usafi wa Mazingira Manispaa ya Shinyanga Snatus Kuchibanda (katikati) akionesha mbolea inayotokana na tope Kinyesi
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania , Wiebe De Boer akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA, Bi. Mwamvua Jilumbi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Afisa kutoka Shirika la SNV (Country Director SNV- Tanzania) , Duncan Rhind akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania , Wiebe De Boer akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kulia) wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Lori likimwaga majitaka katika Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Muonekano eneo la Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Muonekano eneo la Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Muonekano eneo la Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Picha ya kumbukumbu baada ya uzinduzi wa Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi
Picha ya kumbukumbu baada ya uzinduzi wa Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi.
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog