WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dk.Doroth Gwajima akiwa amembeba mtoto mara baada ya kuwasili katika makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dk.DorothA Gwajima,akizungumza na Wazee wakati wa ziara yake ya kikazi katika makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dk.Doroth Gwajima,akiteta jambo na wanafunzi wanaosoma kozi ya ushonaji wanaolelewa katika makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Mwanaidi Ally Khamis ,akizungumza na Mzee aliyepo katika makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Mwanaidi Ally Khamis,akizungumza na wanafunzi wanaosoma kozi ya ushonaji waliopo katika makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma.
Sister wa makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy,Sister Radience,akitoa risala kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dk.Doroth Gwajima (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kutembelea makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dk.Doroth Gwajima,akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi katika makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Mwanaidi Ally Khamis,akitoa wito mara baada ya kutembelea makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt Zainabu Chaula,akizungumzia lengo la ziara hiyo katika makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju,akizungumzia lengo la ziara hiyo katika makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Best Magoma ambaye alikuwa mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akitoa salamu katika makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dk.Doroth Gwajima (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dk.Doroth Gwajima,akiwa akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi katika makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dk.Doroth Gwajima,amesema kuwa takwimu zinaonesha waathirika wakubwa wa vitendo vya ukatili kwa upande wa watoto asilimia 70 ni wa kike.
Pia amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wake wote itaendelea kuimarisha utekelezaji wa afua zenye kuhamasisha kuzuia na kushughulikia aina zote za ukatili ili kuhakikisha jamii ya kitanzania inafurahia haki ya kuishi.
Hayo ameyasema leo Januari 25,2021 mara baada ya kufanya ziara katika makao ya watoto na makazi ya wazee cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo Jijini Dodoma
Waziri Gwajima amesema kuwa, watoto wanapokuwa wanaishi kwenye mazingira hatarishi pamoja na changamoto nyingi pia wanakutana na ukatili mkubwa.
Aidha, ukatili wa majumbani ni sababu mojawapo inayowafanya watoto wakimbilie mitaani na matokeo yake wanakutana na aina zingine za ukatili na mazingira hatari zaidi.
“Ili tuweze kupunguza kadhia hii, silaha ya kwanza ya jamii ni uelewa wa pamoja na kukataa kwa Nguvu moja, kuweka mifumo madhubuti ya kuzuia vitendo vya ukatili” amesema Mhe. Gwajima.
“Pamoja na serikali na wadau wake kuendelea kupambana kuzuia ukatili pia inatoa huduma kwa wahanga wa ukatili ikiwemo huduma ya kisheria ambapo kwa mwaka 2020/21 mashauri 3889 yamepelekwa Mahakamani na 1,504 yametolewa hukumu na mengine kazi inaendelea,”amesema
Aidha, ukiacha ukatili kwa watoto hata watu wazima wanafanyiwa ukatili ambapo wanawake wanatengeneza asilimia 96 ya wanaoathirika.
“Kwa ujumla wake ukatili kwa mtu yeyote haukubaliki, hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau wake wote itaendelea kuimarisha utekelezaji wa afua zenye kuhamasisha kuzuia na kushughulikia aina zote za ukatili ili kuhakikisha jamii ya kitanzania inafurahia haki ya kuishi.
Kwa upande wake,Naibu Waziri Mhe. Mwanaidi Ali Khamis, amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuamka na kufanya kazi yao waliyokusudiwa.
“Upendo unahitajika sana ndio maana Mwalimu Nyerere na Karume waliona umuhimu wa kuanzisha vituo hivi.Maafisa Maendeleo ya Jamii kwa sasa hawana kazi sasa kazi imeanza Rais anataka kuona tunafanya kazi kutembea na kuona uhalisia,”amesema.
Naye,Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dk.Chaula ,ameitaka jamii kutumia rasilimali zilizopo maeneo yao kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kuongeza kipato na kuwasaidia wahitaji, huku akitolea mfano Bwawa la Hombolo na wewe jinsi linavyoweza kuwa mkombozi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo mpya, Amon Mpanju ametoa rai kwa wananchi kuwa na moyo wa kujitolea kuwasaidia wahitaji kwa namna mbalimbali.
Awali akiwasilisha taarifa ya makao hayo kwa Mhe. Waziri, msimamizi msaidizi wa makao hayo Mtawa Radienince MC, amesema makao hayo yana uwezo wa kuhudumia watoto 40 na waliopo ni 23. Aidha Wazee wanaohudumiwa kwa sasa ni 58.
Sista Radience amesema lengo la kuanzishwa kituo ni kuhudumia kutoa huduma kwa maskini bila ya kubagua dini wala ukabila ambapo walengwa hupatiwa huduma zote bure.
Amesema wanakabiliwa na changamoto za gharama kubwa za uendeshaji wa kituo malipo kwa ajili ya umeme na wale ambao wanaumwa hivyo wameomba wapatiwe Solar pamoja na bima ya afya.