Waziri wa nishati , January Makamba akizungumza katika kikao hicho jijini Arusha
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakiwa katika hafla ya kusaini mkataba wa huduma ya ushauri elekezi katika mradi wa LNG jijini Arusha
……………………………………………..
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha .Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia shirika la maendeleo la Petroli nchini ( TPDC )na Kampuni ya Baker Botts (UK)LLP wametia saini mkataba wa huduma ya ushauri elekezi katika mradi wa LNG kwenye maeneo iliyogundua gesi asili .
Mkataba huo umeshuhudiwa leo jijini Arusha na Waziri wa Nishati January Makamba ambapo amesema kuwa ,mchakato wa manunuzi ya mshauri mwelekezi yamefanyika Kwa mujibu wa Sheria na kanuni za nchi ambapo Kampuni hiyo ilifanikiwa kushinda zabuni hiyo.
Amesema kuwa,mchakato huo umetokana na nia njema ya serikali ya awamu ya sita kuhakikisha kwamba majadiliano ya kumpata mzabuni yanamalizika kwa haraka na kumpata mwenye uzoefu mkubwa katika miradi ya aina hii.
“Kama mnavyofahamu serikali iligundua kiasi kikubwa cha gesi asilia katika kina cha maji marefu katika vitalu namba moja ,mbili na nne ndio maana imeona umuhimu wa kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kampuni zenye uzoefu ni muhimu “amebainisha Makamba.
Amefafanua kuwa, kama ilivyo utaratibu wa kimataifa katika maswala ya majadiliano wa miradi mikubwa kama hii ya kusindika na kuchakata gesi asilia kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi yameona umuhimu wa kupata mshauri mwelekezi kama lampuni hii ambayo serikali imeingia nayo mkataba.
Aidha amebainisha kuwa, serikali na kampuni zilizogundua gesi hiyo zilianza majadiliano kutoka November 8/2021 kwa kutumia wataaalamu wa ndani Kama ilivyo utaratibu wa kimataifa katika maswala ya majadiliano ya miradi mikubwa ushauri wa kitaalamu kutoka Kampuni zenye uzoefu ni muhimu Ili kufikia malengo .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la maendeleo ya Petrol ,James Mataragio amesema kuwa, taasisi hiyo itasaidia sana serikali katika miradi ya kimkakati na kuongoza serikali kupata manufaa katika rasilimali ya mafuta na gesi.
Amesema kuwa ,tumefikia makubaliano haya kuongeza ufanisi utakaosaidia uzoefu wa wenzetu kuingia katika mikataba mbalimbali na kampuni za ndani na nje ya nchi Ili itupatie tija katika matumizi ya rasilimali mafuta.