Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala (katikati) akifafanuliwa jambo na Msemaji wa Uhamiaji Mrakibu Paul Mselle (kushoto) wakati wa kikao cha utambulisho walipotembelewa na Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Puyo Nzalayaimisi (wa pili kulia), leo tarehe 24 Januari, 2022 Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji Dodoma.
Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Puyo Nzalayaimisi (kushoto) akipokelewa na Msemaji wa Uhamiaji Mrakibu Paul Mselle (kulia) mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji Dodoma leo tarehe 24 Januari, 2022.
Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Puyo Nzalayaimisi (kushoto) wakiteta jambo na Msemaji wa Uhamiaji Mrakibu Paul Mselle (kulia) katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji Dodoma leo tarehe 24 Januari, 2022.
(Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
**************************
Msemaji Mpya na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Puyo Nzalayaimisi leo tarehe 24 Januari 2022 amefanya ziara ya kujitambulisha na kuongeza uhusiano baina ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Jeshi la Uhamiaji nchini katika Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dodoma.
SACF Nzalayaimisi alipokelewa na Msemaji wa Uhamiaji Mrakibu Paul Mselle na baadae kukutana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala kwa ajili ya kujitambulisha.
Dkt. Makakala amempongeza SACF Nzalayaimisi kwa kuteuliwa nafasi ya kuwa Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kumtakia mafanikio mema katika kutekeleza majukumu yake kwa manufaa ya Taifa.
Aidha Kamishna Jenerali Dkt. Makakala amevitaka vitengo vya Habari Mawasiliano na Uhusiano katika majeshi hayo kuendeleza uhusiano na ushirikiano ili kubadilishana uzoefu katika kazi mbalimbali za kihabari.
Kwa upande wake Msemaji Mpya wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji SACF Puyo Nzalayaimisi, amelishukuru Jeshi la Uhamiaji kwa kuimarisha uhusiano uliopo wa kutekeleza majukumu ya habari na elimu kwa umma kupitia mitandao ya kijamii na kuahidi kwamba wataendelea kujifunza namna Jeshi la Uhamiaji linavyotekeleza majukumu yake ya kuhabarisha umma kupitia mitandao ya kijamii na njia nyingine mbalimbali za kidijitali.