Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wakati alipowasili katika kijiiji cha Matufa kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Darakuta- Magugu – Mwada uliopo Babati Vijijini mkoani Manyara,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi wa Maji Darakuta – Magugu – Mwada uliopo Babati Vijijini mkoani Manyara, Januari 25, 2022. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mbunge wa Babati Vijijini, Daniel Siro, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimbi na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Manyara, Simon Lulu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua chujio la maji katika chanzo cha maji cha Mradi wa maji Darakuta – Magugu – Mwada uliopo Babati Vijijini mkoani Manyara kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo, Januari 25, 2022. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji wa Mji wa Babati, Mhandisi Iddy Msuya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubebe ndoo ya Maji, Mwnaharusi Swaleh wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Darakuta – Magugu – Mwada uliopo Babati Vijijini mkoani Manyara, Januari 25, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)