**********************
Happy Lazaro, Arusha
Arusha.Katibu Mkuu wa wizara ya habari,mawasiliano na teknolojia ya habari ,Dokta Jim Yonazi amewataka maafisa Tehama nchini kuwa wabunifu pamoja na kujifunza kila wakati ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia yanayojitokeza kila wakati.
Ameyasema hayo leo jijini Arusha katika kikao cha wadau wa mawasiliano Serikalini kilichowashirikisha wakurugenzi wa Tehama wa wizara zote nchi nzima na wakurugenzi wa rasilimali watu nchi nzima kujadilii ya mahitaji ya taaluma ya Tehama yanayotekelezwa katika mradi wa Tanzania ya kidigitali.
Amesema kuwa, kutokana na mabadiliko ya teknolojia ya Tehama duniani Kila wakati inahitajika kutoa mafunzo ya mara kwa mara kuongeza ujuzi ili kwenda na kasi ya mabadiliko hayo.
“Mafunzo haya yaende sambamba na mageuzi ya teknolojia na uharaka wake duniani kwa kujenga na kuongeza vituo vya malipo ya serikali kwa njia ya kidigitali utakaosaidia wananchi kupata huduma hiyo popote walipo”amesema Yonazi.
Mratibu wa mradi wa Tanzania ya kidigitali wizara ya habari mawasiliano na teknolojia ya habari, Honest Njau amesema kuwa, mradi huo unagharimu takribani Dola za kimarekani 150 milioni sawa na fedha za kitanzania bilioni 349 na ulishaanza tangu mwaka Jana utatekelezwa ndani ya kipindi cha miaka 5.
Amesema kuwa ,serikali ipo mbioni kujenga minara ya mawasiliano mia nne ya kimkakati nchini ikiwa ni maboresho ya kuendana na matumizi ya internet hususani maeneo yenye upungufu wa mawasiliano ya Internet vijijini.
“Tupo mbioni kujenga zaidi ya minara 400 kutoka 2G kwenda 4G Ili kuendana na kasi ya matumizi ya internet huko vijijini ambapo mawasiliano ya aina hiyo hamna nayanachelewesha ujenzi wa uchumi na maendeleo ya mawasiliano”
Mradi huo ulianza mwaka jana utatekelezwa Kwa kipindi Cha miaka mitano ukiwa na malengo matatu ikiwemo kujengea uwezo wataaalam wa Tehama ,kupeleka huduma za Serikali karibu na wananchi ili kumueezesha mwananchi kupata huduma kiuraisi ikiwemo pia ujenzi wa minara ya mawasiliano hususa ni sehemu zenye Mapungufu.