WAZIRI wa Madini Dotto Biteko,akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) Bi.Salma Ernest alipowasili kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) uliofanyika leo Januari 24,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Madini Dotto Biteko,akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kondoa Mhe.Khamis Mkanachi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alipowasili kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) uliofanyika leo Januari 24,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Dotto Biteko,akishuhudia Mkataba wa makubaliano kati ya CRDB na STAMICO Mkurungenzi wa wateja wakubwa na Serikali wa Benki ya CRDB, Prosper Nambaya (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dk Venance Mwasse wakitiliana saini mkataba wa makubalino baina ya pande hizo mbili kwaajili ya mikopo ya wachimbaji wadogo Tanzania. Wanaoshuhudia kushoto ni Mwanasheria wa STAMICO, Robert Ambrose na Meneja Mahusiano Idara ya Wateja wakubwa wa Benki ya CRDB, Alex Rwegayura. Mkataba huo ulisainiwa Jijini Dodoma leo Januari 24,2022 wakati wa Mkutano wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimba Madini Tanzania (TAWOMA).
WAZIRI wa Madini Dotto Biteko,akizungumza na washiriki wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) uliofanyika leo Januari 24,2022 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Madini Dk.Stephen Kiruswa,akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) uliofanyika leo Januari 24,2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa TAWOMA Bi.Gilly Rajab ,akizungumzia lengo la Mkutano huo katika Mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) uliofanyika leo Januari 24,2022 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dk Venance Mwasse akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) uliofanyika leo Januari 24,2022 jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kondoa Mhe.Khamis Mkanachi,akitoa salamu za Mkoa wakati wa Mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) uliofanyika leo Januari 24,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) Bi.Salma Ernest,akisoma risala wakati wa Mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) uliofanyika leo Januari 24,2022 jijini Dodoma.
Mkurungenzi wa wateja wakubwa na Serikali wa Benki ya CRDB, Prosper Nambaya akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) uliofanyika leo Januari 24,2022 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Madini Dotto Biteko,(hayupo pichani ) i wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) uliofanyika leo Januari 24,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Madini Dotto Biteko,akizindua WORTH YETU mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) uliofanyika leo Januari 24,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Madini Dotto Biteko,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) uliofanyika leo Januari 24,2022 jijini Dodoma.
……………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Madini Dotto Biteko,amezitaka taasisi za kifedha kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo wanawake kwakua ni waaminifu katika masuala ya fedha kuliko wanaume.
Dk.Biteko ameyasema leo Januari 24,2022 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) ambapo amesema wanawake wana nafasi kubwa katika kuitumikia sekta ya madini nchini kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Aidha,amezitaka taasisi za kisekta ya madini pamoja na makampuni ya madini nchini kuwaamini wanawake katika shughuli za Madini kwani wana uaminifu mkubwa ikilinganishwa na wanaume.
“Simaanishi kuwa wanaume siyo waaminifu lakini wanawake kuna kitu mungu amewapa ambacho sisi wanaume hatuna, hata takwimu za watu ambao wanaotorosha madini idadi kubwa ni wanaume wanawake ni wawili tuu hadi sasa”amesema Biteko
Dk.Biteko amewataka wanawake nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika shughuli za uchumbaji madini badala ya kuendelea kubaki nyuma katika sekta hiyo inayochangia kiasi kikubwa katika pato la taifa.
“Mnapaswa kuwa kinara kwenye madini acheni kujiona duni kwani sekta ya madini si kwa ajili ya wanaume tuu shughuli za uchimaji hata nyie mnaweza kuzifanya tena kwa ufanisi mkubwa”amesema Biteko
Aidha amesema kuwa wanawake hawapaswi kuwa sehemu ya watizamaji katika sekta hiyo bali kuwa mstari wa mbele katika kushiriki shughuli za uchimbaji na kutoa mchango katika ukuzaji wa pato la taifa kupitia sekta hiyo.
“Tuondoe dhana ya kwamba shughuli za uchimaji wa madini ni za wanaume na anayepaswa kupewa leseni za uchimaji ni mwanaume hapana wanawake wakiiingia katika sekta hii sehemu kubwa ya jamii itanufaika na sekta hii ya madini”amesema Biteko
Waziri Biteko, amesema serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wanawake wachimbaji wa madini ili kuzifikia ndoto zao.
“Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo katika sekta hii hivi sasa hata katika usafirishaji wa madini watanzania wanahusika, zamani ilikuwa ukitaka uchimbe madini hadi mtu fulani aseme”amesema
Kwa upande wake Naibu waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema mkakati wa serikali ni kuhaikisha wachimbaji wadogo wananufaika pamoja na kupewa elimu ya teknolojia bora ya uchimbaji wa madini.
”Shirika la madini la taifa (STAMICO) ndio lenye wajibu wa kuhakikisha wachimbaji wanakuwa na tija katika uchimbaji huku akisisitiza wachimbaji wote wa madini kujisajili.”amesema Dk.Kiruswa
Awali Katibu Mkuu wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) Bi.Salma Ernest,akisoma risala amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa wataalam wa masuala ya madini.
“Changamoto nyingine mgeni rasmi ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kisasa kwa ajili ya uchimbaji madini,teknolojia ya uchenjuaji, ukosefu wa umeme katika maeneo ya uchimbaji lakini pia kukatikatia kwa umeme mara kwa mara katika maeneo ya uchimbaji madini”amesema Ernest