………………………………………………..
SPIKA Mstaafu Anne Makinda amesisitiza kuwa sensa ya watu na makazi mwaka huu ni muhimu kwakuwa itawezesha serikali kujua idadi ya watu kila eneo na kuzingatia ugawaji mapato
Anne ambaye pia kamisaa wa sensa ya watu na makazi na mjumbe wa jumuiya ya maridhiano Tanzania aliitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa amani uliojumuisha viongozi mbalimbali ambapo alitumia nafasi hiyo kueleza namna sensa inavyoweza kuhamasisha ulipaji kodi kwa wananchi kama ikitumika vizuri.
“Tumeelezwa na mtu wa TRA kwamba mpaka mwaka juzi waliokuwa wanalipa kodi halali walikuwa milioni 3 kati ya milioni 60 hivyo ubunifu uliofanywa na serikali kupata hiyo
…Mwaka huu ni wa sensa ya taifa ya kuhesabu watu na makazi yao faida ya kufanya hiyo kitu kwa sababu leo sisi tuna watoto wengine walemavu wamefichwa majumbani hawajulikani, kuna wazee wanamuomba Mungu tuu awanusuru, kuna watu wenye matatizo chungu nzima…
Ukiingia kwenye vyombo vya habari utakuta mtu anaomba kitu mpaka unasikia uchungu lakini sisi watanzania tupo,”alisema Anna.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA, Richard Kayombo
alieleza kuwa nchini kuna ukanda mrefu wa bahari, maziwa na kumepakana nan chi nane hivyo kuna vichochoro vingi vya magendo ambavyo vinanufaisha baadhi ya watu na kusababisha ukusanyaji mapato kutoongezeka wakati lengo la kufikia zaidi ya sh. Trilioni 3 lipo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum, amesema kulipa kodi ni ibada na kukwepa kulipa kodi ni dhambi huku akiwataka wanamaridhiano wote nchini kuunga mkono juhudi za serikali kuhusu suala hilo ili nchi iendelee.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda aliipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kutumia viongozi wa dini kuelimisha waumini na watanzania kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.