Mkurungenzi wa wateja wakubwa na Serikali wa Benki ya CRDB, Prosper Nambaya (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dk Venance Mwasse wakitiliana saini mkataba wa makubalino baina ya pande hizo mbili kwaajili ya mikopo ya wachimbaji wadogo Tanzania. Wanaoshuhudia kushoto ni Mwanasheria wa STAMICO, Robert Ambrose na Meneja Mahusiano Idara ya Wateja wakubwa wa Benki ya CRDB, Alex Rwegayura. Mkataba huo ulisainiwa Jijini Dodoma leo Januari 24,2022 wakati wa Mkutano wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimba Madini Tanzania (TAWOMA).
Mkurungenzi wa wateja wakubwa na Serikali wa Benki ya CRDB, Prosper Nambaya akitia saini kwa niaba ya Benki ya CRDB ambayo imekusudia kuwakopesha Wachimbaji wadogo. Jambo ambalo litawezesha wachimbaji hao kupata mitaji na kufanya kazi zao za uchimbaji wenye tija.
Mkurungenzi wa wateja wakubwa na Serikali wa Benki ya CRDB, Prosper Nambaya (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dk Venance Mwasse wakibadilishana mkataba wa makubalino baina ya pande hizo mbili waliosaini kwaajili ya mikopo ya wachimbaji wadogo Tanzania. Wanaoshuhudia kushoto ni Mwanasheria wa STAMICO, Robert Ambrose na Meneja Mahusiano Idara ya Wateja wakubwa wa Benki ya CRDB, Alex Rwegayura. Mkataba huo ulisainiwa Jijini Dodoma leo
Januari 24,2022 wakati wa Mkutano wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimba Madini
Tanzania (TAWOMA).
Wabunge wanawake walioshiriki mkutano Mkutano wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimba Madini Tanzania (TAWOMA) jijini Dodoma leo Januari 24,2022.
Viongozi wa Benki ya CRDB wakifuatilia matukio
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dk Venance Mwasse akizungumza baada ya kutiliana saini na Benki ya CRDB.
Wanachama wa TAWOMA wakifuatilia kwa makini matukio katika mkutano wao.
Mkurungenzi wa wateja wakubwa na Serikali wa Benki ya CRDB, Prosper Nambaya akizungumza na baada ya kuingia makubaliano na Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) jijini Dodoma leo ambapo CRDB itakua ikikopesha fedha kwa wachimbaji wadogo nchini Tanzania.
Wabunge wanawake walioshiriki mkutano Mkutano wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimba Madini Tanzania (TAWOMA) jijini Dodoma leo Januari 24,2022.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha Zeytun Swai akifuatilia mkutano huo wa Mkutano wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimba Madini Tanzania (TAWOMA) jijini Dodoma leo Januari 24,2022.
Wabunge wanawake walioshiriki mkutano Mkutano wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimba Madini Tanzania (TAWOMA) jijini Dodoma leo Januari 24,2022.
Wanachama wa TAWOMA wakifuatilia kwa makini matukio katika mkutano wao.
……………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
BENK ya CRDB imesaini mkataba wa makubaliano (MoU) na Shirika la Madini Taifa (STAMICO) kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo huku ikisema ipo tayari kuwahudumia wachimbaji hao.
Akizungumza leo Januari 24,2022,katika mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimba Madini Tanzania (TAWOMA) Mkurungenzi wa wateja wakubwa na Serikali wa Benki ya CRDB, Prosper Nambaya amesema wanaamini makubaliano hayo yatakuwa ni endelevu.
Amesema Benk ya CRDB imejikita katika mambo ya madini ambapo mpaka sasa imefanikiwa kutoa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 100 huku akidai kubwa ambayo wamekuwa wakikutana nayo ni jinsi ya kuwafikia wachimbaji wadogo.
“Mimi ninachoomba na ninachosisitiza kutokana na haya makubaliano tuliosaini leo hii inatakiwa yawe endelevu na pia tutakaa tuone tutafanyaje urasimishaji wa hawa wachimbaji wadogo ni ngumu sana kama Benk kwenda kufainance mtu mmoja mmoja,”amesema.
Amesema sasa ni muda muafaka kukaa na kusonga mbele kwa ajili ya kumsaidia mchimbaji mdogo aweze kukopesheka ili ajikwamue kiuchumi.
“Kwanini tumepata mfumo kama mkulima wa pamba mdogo anataka anunue mbolea,madawa mkulima yule anajulikana kwanini tusifanye hivyo kwenye madini?amehoji Nambaya.
Mkurugenzi huyo amesema CRDB ipo tayari kuwahudumia wachimbaji wadogo nchini kutokana na kuwa na kanda saba katika maeneo mbalimbali Nchini.
“Ninachoomba kwa kupitia huu ushirikiano tupo tayari kama CRDB kuwahudumia Nchi nzima tuna zone 7 kupitia ule mfumo tutakapoelewana utakuwa ni wakati muafaka watu kutembeelea zile zone.Na kama tunavyosema CRDB kauli mbiu yetu ulipo tupo huku juu tumefanikiwa sasa tuende chini,”amesema.