Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezi ya Wizara na Idara za Serikali nchini (SHIMIWI), Moshi Makuka (mwenye miwani) akielezea masuala mbalimbali yanayohusiana na uchaguzi kwa wajumbe walioshiriki mkutano mkuu wa dharura wa shirikisho hilo (hawapo pichani) uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.
Wajumbe kutoka Wizara na Idara mbalimbali za serikali wakiwa kwenye mkutano wa dharura wa Shirikisho la Michezi ya Wizara na Idara za Serikali nchini (SHIMIWI), uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.
Wajumbe wa Mkutano wa dharura wa Shirikisho la Michezi ya Wizara na Idara za Serikali nchini (SHIMIWI), wakimsikiliza mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo, Assumpta Mwilanga (aliyesimama mbele) wakati akijitambulisha kwenye mkutano huo uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezi ya Wizara na Idara za Serikali nchini (SHIMIWI), Ally Katembo (aliyesimama mbele) akisistiza jambo kwa wajumbe walioshiriki mkutano wa dharura wa shirikisho hilo (hawapo pichani) uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.
Wajumbe wa Mkutano mkuu wa dharura wa Shirikisho la Michezi ya Wizara na Idara za Serikali nchini (SHIMIWI),uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma wakiendelea kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo ambao unatarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.
……………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
ALIYEWAHI kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kwenye Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leonard Thadeo pamoja na Hakimu Mfawidhi mstaafu wa Mahakama ya Utete, Rufiji, Ally Katembo ni miongoni mwa wajumbe watano walioteuliwa kuunda kamati ya kusimamia uchaguzi wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali nchini (SHIMIWI), unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu kwenye mkoa utakaotangazwa baadae
Wanakamati hao wamepitishwa jana kwenye mkutano mkuu wa dharura wa SHIMIWI uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma, ambapo wanakamati wengine walikopitishwa kwa kura za ndio za wajumbe wote 98 walioshiriki ni Joyce Benjamin mstaafu aliyekuwa mtumishi wa Umma kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, huku Mohamed Ally aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Uchukuzi na sasa ni Mkurugenzi wa Utawala kwenye Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) na Thadeo Almas ambaye ni Mwanasheria wa baraza la Michezo la Taifa (BMT). Mohamed ndio Katibu wa kamati hiyo ambapo Mwenyekiti ni Mwanasheria.
Akizungumza kwenye mkutano huo Katibu Mkuu mstaafu wa SHIMIWI, Moshi Makuka amesema kwa mujibu wa katiba ya shirikisho hilo Ibara ya 21 inataka Mwenyekiti wa Kamati hiyo lazima awe na taaluma ya Sheria; ambapo kwa ujumla aliyataja majukumu ya kamati hiyo kuwa ni pamoja na kushughulikia masuala yote yanayohusu uchaguzi wa shirikisho; kuandaa kanuni za uchaguzi na kuziwasilisha kwa Kamati ya Utendaji ili zipitishwe na Mkutano Mkuu; na kutoa fomu za kugombea nafasi mbalimbali
Majukumu mengine ni kufanya usaili wa wagombea; kutangaza majina ya wagombea; kupanga tarehe ya uchaguzi kwa wakishirikiana na Kamati ya Utendaji iliyopo madarakani; kusimamia uchaguzi na kutangaza matokeo ya uchaguzi
Mbali na uteuzi huo wa wajumbe, pia wajumbe hao wamepitia na kuboresha kanuni za uchaguzi, ambazo zinaonesha taratibu za uchaguzi huo; kuchambua, kutangaza majina ya wangombea; wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi na wenye haki ya kupiga kura; wagombea kujieleza; wajumbe wenye haki; kupiga kura; mpangilio wa uchaguzi; kuhesabu kura; mshindi; na matokea ya uchaguzi.
Hatahivyo, Makuka amezitaka klabu zote ambazo bado kufanya uchaguzi zihakikishe zinakamilisha zoezi hilo, ili waweze kupata nafasi ya kuingia kwenye mkutano wa uchaguzi mkuu kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi; pia wahakikishe wanachagua viongozi makini, wenye weledi, busara na ushawishi kwa viongozi mbalimbali wa ngazi za juu.
“Pia mkahikishe mnatengeneza bajeti halisia kwa ajili ya mabonanza na mashindano zikiwa na tija kwa wizara na Idara za serikali, kwani itasaidia kufanya uongozi ujipange kwa ufanisi na kuweza kushiriki kila wakati bila kukosa fedha za ushiriki,” amesema Makuka.
Naye Mwenyekiti wa mkutano huo wa dharura, Ally Katembo amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.\
MWISHO