*******************
23,Jan
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae pia ni naibu Waziri wa ardhi,amepita Kutoa Mkono wa Pole kwa wahanga wa Majanga ya Mvua na Upepo, Kijiji cha Makombe na Mji wa Bwilingu,ambapo pia amechangia milioni tano katika mfuko wa maafa.
Mvua kali iliyoambatana na Upepo mkali imeleta maafa katika baadhi ya maeneo Chalinze Mkoani Pwani, na kuezua paa za Nyumba zaidi ya 35 na madarasa , na kuwaacha wananchi katika tabu kubwa.
” Tumekubaliana kuwa ndani ya Wiki hii Shule iwe imerudi katika hali yake na kwa wananchi taratibu zinafanywa kuwapatia misaada mbalimbali ikiwemo vyakula na mahitaji muhimu ya kibinadamu.
“Nimechangia shilingi Milioni 5 mfuko wa maafa ili kupunguza makali ya Madhara hayo.”alifafanua Ridhiwani.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Ramadhani Possi alisema hatua inayoendelea ni tathmini na baada ya tathmini fedha itatolewa hususan kutatua madhara upande wa sekta ya elimu kwenye Madarasa yaliyoezuliwa shule ya msingi Makombe.