Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akiwa pamoja na ujumbe alioambatana nao kutoka Tanzania wakiwa katika moja ya banda la Tanzania wakiwa na mmiliki wa Kampuni ya uwindaji wa Kitalii anayemiliki vitalu vya uwindaji nchini Tanzania, Adam Clements (wa pili kulia) akiwaonesha kwenye kompyuta mpakato moja ya vitalu hivyo anavyovimiliki mara baada ya Waziri kumtembelea kwa lengo la kujifunza na kusikia changamoto anazokabiliana nazo katika katika banda lake ikiwa ni miongoni mwa Makampuni nane kutoka Tanzania yaliyoshiriki katika mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention) ulioanza rasmi leo katika Jiji la Las Vegas, Nevada nchini Marekani. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa TAWA, Brigedia Jenerali,( Mst.) Hamisi Semfuko apamoja na Balozi wa Tanzania Nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (wa tatu kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA, Brigedia Jeneralia (Mst.) Hamisi Semfuko ( watatu kulia) wakipata maelezo kutoka kwa moja ya Wenyeji wa Mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention), Judith Henkel (wa kwanza kulia) akiwa na mwenzake Anna Saint (wa pili kulia) jinsi wanavyopata Washiriki wa Maonesho ya Uwindaji wa Kitalii yanayoendelea kufanyika katika Jiji la Las Vegas, Nevada nchini Marekani. Wengine ni Wajumbe aliombatana nao kutoka kutoka Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akiwa pamoja na ujumbe aliombatana nao kutoka Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na mmoja ya Wadau wa Uwindaji wa Kitalii John James pamoj na mkewe Julieth Nathians ikiwa ni miongoni mwa Makampuni nane kutoka Tanzania yaliyoshiriki katika mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention) unaoendelea kufanyika katika Jiji la Las Vegas, Nevada nchini Marekani. Wa nne kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza, wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Brigedia Jeneral,(Mst) Hamisi Semfuko
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (wakwanza kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA, Brigedia Jeneralia (Mst.) Hamisi Semfuko ( wa pili kushoto ) wakipata maelezo kutoka kwa Mmiliki wa Kampuni ya Uwindaji wa Kitalii, Bw. Adam Clements ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Uwindaji wa Kitalii ya Adam Clement Safari kutoka Tanzania akiinadi Tanzania katika Mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii katika Maonesho ya Uwindaji wa Kitalii yanayoendelea kufanyika katika Jiji la Las Vegas, Nevada nchini Marekani. Wa pili tatu kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( wa pili kulia ) akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza ( wa kwanza kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwindaji wa Kitalii ya Detail Macclum Safari, Mike Angelides ambaye ni miongoni mmiliki wa vitalu vya uwindaji nchini Tanzania aliyeshiriki katika Maonesho yanayofanyika wakati wa Mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention) ulioanza rasmi kufanyika leo katika Jiji la Las Vegas, Nevada nchini Marekani. Wa pili kusho ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TAWA, Brigedia Jenerali (Mst.) Hamisi Semfuko
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akiwa pamoja na ujumbe aliombatana nao kutoka Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na mmiliki wa Kampuni ya uwindaji wa Kitalii ya Headlands Bw. Rack Ramadhan (wa kwanza kulia) ambaye ni mmiliki wa vitalu vya uwindaji wa kitalii nchini Tanzania, ikiwa ni miongoni mwa Makampuni nane kutoka Tanzania yaliyoshiriki katika mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention) unaoendelea kufanyika katika Jiji la Las Vegas, Nevada nchini Marekani
…………………………………………………..
Na Mwandishi Maalum, Las Vegas, Marekani
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ametoa ahadi ya kukutana na Wadau wa Uwindaji wa Kitalii wanaomiliki Vitalu vya Uwindaji nchini Tanzania ambao sio wanachama wa Chama cha Uwindaji wa Kitalii Tanzania (TAHOA), Mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu.
Kauli hiyo ameitoa leo Jijini hapa Las Vegas Nevada, Marekani wakati akitoa wito kwa Kamati ya watu 10 aliyoiounda kwa ajili ya kumshauri yeye kama Waziri namna bora ya kuendesha sekta ya uwindaji ya kitalii kuwasilisha ripoti itakayomsaidia kuboresha minada ya kielektroniki ya Biashara ya uwindaji wa Kitalii inayofuata hapo baadae.
Dkt. Ndumbaro amesema kuwa, mkutano huo utakuwa na lengo la kuboresha mazingira ya biashara ya sekta hiyo ikiwemo uzoefu walioupata katika ushiriki wa Maonesho ya 50 ya mwaka ya Uwindaji wa Kitalii yanayoendelea yakiwakutanisha watunga sera na wafanya maamuzi kutoka nchi mbalimbali Duniani juu ya kuendeleza sekta ya uwindaji.
Akizungumzia juu ya Kamati aliyoiunda Juni 23, 2021 Jijini Dodoma ya watu 10 ikiwa na watu watano kutoka Sekta binafsi na wengine watano kutoka Serikalini kushindwa kuwasilisha ripoti ya ushauri huo hadi leo.
Dkt. Ndumbaro amewataka Wadau hao wanaomiliki vitalu vya uwindaji vya kitalii nchini Tanzania kuacha kulalamika baadala yake wawasilishe ripoti hiyo ya ushauri kwa kuonesha yale waliyokubaliana kwa pamoja na yale waliyotofautiana ili yeye kuifanyia kazi ripoti hiyo
Amesema kitendo cha Kamati hiyo kushindwa kuiwasilisha ripoti hiyo kwa wakati kumempelekea yeye kama Waziri katika wakati mgumu katika kufanya maamuzi yenye maslahi mapana pande zote mbili yaani kwa Serikali na Wadau wa Sekta hiyo.
Amesema kuwasilishwa kwa ripoti hiyo mapema kutatoa muelekeo wa namna bora ya kuendesha minada ya kielektoniki ya Uwindaji wa Kitalii inayofuata katika mazingira bora zaidi.
“Baadhi yenu mmekuwa mkilalamika tu kuwa hamtaki minada wa kielektoniki wa vitalu vya uwindaji wa Kitalii, leteni ushauri kupitia ripoti hiyo mkionesha sababu na njia mbadala kama Serikali nini tufanye” alisema Dkt. Ndumbaro.
Kufuatia hali hiyo, Dkt.Ndumbaro amewasisitiza Wadau hao waliopo nchini Marekani ambao ni Washiriki wa Maonesho hayo 50, kuiwasilisha ripoti hiyo mapema iwezekanavyo ili mwanzoni mwezi Februari aweze kuitisha mkutano wa Wadau hao.
Hata hivyo, Dkt. Ndumbaro amewapongeza Wadau hao kwa maoni mazuri waliyoyatoa katika kikao alichofanya nao nchini hapa huku akiwasisitizia kuuweka ushauri huo katika maandishi na kuwasilisha ofisini kwake kwa lengo kuiwezesha Serikali na wadau hao kunufaika kupitia Biashara hiyo.
Awali, Mwenyekiti wa Chama cha Uwindaji wa Kitalii (TAHOA), Michel Matheakis alimshukuru Waziri kwa kuwa muumini wa mazungumzo na kuahidi kuwa ripoti hiyo itawasilisha kwa ajili ya kufanyiwa kazi.