Mh Neema Lugangira akiwa katika moja ya vikao vyake na Wavuvi wa Bukoba Manispaa mwaka 2020
Mwenyekiti wa Chama Cha Wavuvi Mkoa wa Kagera Ndg. Merdad Kaijage akizungumza wakati wa mkutano huo
Katibu Alex Bakenjela akizungumza wakati wa mkutano huo |
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof Kamuzora akizungumza wakati wa mkutano huo
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof Kamuzora akizungumza wakati wa mkutano huo
NA MWANDISHI WETU, KAGERA
CHAMA
cha Wavuvi Mkoani Kagera kimemchagua Mbunge wa Viti Maalumu kupitia
Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira kuwa mlezi
wa chama hicho wakati wa mkutano mkuu wao uliofanyika Januari 20 mwaka huu.
Akitangaza
uamuzi huo leo wakati wa mkutano mkuu chama hicho uliofanyika katika
Ukumbi wa Linas uliopo Manispaa ya Bukoba ambapo Mwenyekiti wa chama
hicho Merdard Kaijage alisema chama wameazimia kwa pamoja kumpitisha
Mbunge Neema Lugangira kuwa mlezi wao.
Alisema
chama hicho kinahitaji walezi ambao watawasaidia kuendeleza chama na
kuwasemea wavuvi huku akieleza mlezi huyo ni mtu sahihi kwao kuweza kuwa
chachu kubwa ya maendeleo kutokana na mchango mkubwa ambao amekuwa
akiutoa kwa jamii.
Mkutano
huo mkuu ulihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof Kamuzora
ambaye alikuwa mgeni Rasmi wa Mkutano wa Chama Cha Wavuvi Mkoa
Kagera,Mwenyekiti wa Chama Cha Wavuvi, Ndg. Merdad Kaijage, Katibu Alex
Bakenjela, Afisa Ushirika wa Mkoa wa Kagera na Wavuvi ambao ni
Wanachama.
Katika
Mkutano huu chama hicho kilitumia nafasi hiyo kujadili na Kupitisha
Katiba ya Chama n ambayo itakuwa ni silaha kubwa ya kuweza kuendesha
masuala mbalimbali kisheria
Akizungumza
wakati akifungua mkutano huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera ( RAS)
Prof Kamuzora alisema siku zote wavuvi wanafanya kazi zao kwa kujitenga,
hawakuwa na chombo cha kuwaunganisha na Kuwasemea hivyo hatua hii ya
kuwa na Chama Cha Wavuvi Kagera kitasaidia sana kujenga na kuinua Sekta
ya Uvuvi Mkoa wa Kagera.
Alisema
Mkoa wa Kagera una fursa nyingi lakini hazitumiki ipasavyo kuinua
Uchumi wa Kagera hivyo aliahidi kutoa Ushirikiano wa kila hali
utakapohitajika.
Prof
Kamuzora aliwataka wavuvi wawe wamoja kuanzia Wavuvi Ziwani, Wafugaji
wa Samaki pamoja na wanaojishughulisha na Uvuvi Ziwa Burigi huku akitoa
wito kwao kuacha kushiriki kwenye vitendo vya uvuvi haramu.
Kwa
upande wake Katibu wa Chama Cha Wavuvi Kagera, Ndg. Alex Bakenjela
alimuhakikisha Katibu Tawala huyo kuwa chama hiki hakitashirikiana na
Mwanachama yeyote atakaejihusisha na Uvuvi Haramu na watakuwa tayari
kuwafichua watakaobainika kushiriki kwenye vitendo vya namna hiyo
Wajumbe
wa Chama cha Wavuvi Kagera wote kwa pamoja walifunga Mkutano huu kwa
Kumpogeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania kwa kazi nzuri
anayofanya pamoja na Wasaidizi Wake.