Adeladius Makwega ,KILIMANJARO.
Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Pauline Gekul amewashukuru wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro kwa kumpokea vizuri Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mkoani hapo ambaye ndiye Mgeni rasmi wa Tamasha la Utamaduni la Kilimanjaro.
“Tunawashukuru Wanakilimanjaro kwani tumepata baraka kubwa kwa kuwa mvua kubwa zimenyesha katika mapokezi hayo ya mheshimiwa Rais Samia.”
Mheshimiwa Gekul ameyasema hayo kandoni mwa Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi ambapo maandalizi ya mwisho yamekamilika huku akitoa wito kwa wananchi wa mkoa huu kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais Samia katika Tamsha la Utamaduni la Kilimanjaro Januari 22,2022 viwanjani hapo.
“Nawakaribisha Wanakilimanjaro ili wawezi kujumuika na mheshimiwa rais wetu na zile mila zetu nzuri lazima tuziendeleze na maadhimisho haya yanatanyia kila mkoa kwani machifu hawa walituongoza vizuri kabla ya uhuru na walifanya kazi kubwa ya kutukomboa.”
Akiwa katika viwanja hivyo mheshimiwa Gekul amesema kuwa kufanyika kwa matasha haya kuna shabaha kubwa sana kwa taifa letu lengo ni kuhamasisha mambo yote mazuri ya mila zetu yaendelee kufuatwa na jamii zetu.
Naibu Waziri Gekul sambasamba na hayo alipata nafasi ya kuzunguma na Chifu Frank Mareale uwanjani hapo.