Na John Walter-Manyara
Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), umefadhili Minara ya makampuni ya mitandao ya simu 54 katika kata 42 Mkoani Manyara.
Hayo yamesemwa na Mhandisi Mwandamizi wa mfuko wa mawasiliano kwa wote, Baraka Elieza, wakatika akizungumza na Waandishi wa habari Mkoani hapa katika ziara ya Naibu waziri wa habari mawasiliano na teknolojia ya habari amesema kuwa Minara yote walioifadhili imekamilika isipokuwa Minara miwili ambayo itakamilika mapema mwaka huu.
Ameitaja Minara hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika hivi karibuni ni katika Kijiji cha Sigino pamoja na Kijiji cha Himiti.
Akizungumzia mipango ya mfuko huo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), kwa mwaka wa fedha 2021_2022, nikutekeleza ujenzi wa Minara katika kata 15 ndani ya mkoa wa Manyara
Amesema wamejikita katika maeneo ya vijijini na baadhi ya maeneo ya mijini, ambapo Kuna usikivu hafifu wa mawasiliano, kwa kutoa ruzuku kwenye makampuni ya mitandao ya simu ili wapeleke huduma ya mawasiliano kwa wananchi, pamoja nakupeleka mawasiliano ya redioni katika maeneo ambao Kuna usikivu hafifu wa redio.
Aidha mfuko huo unafundisha walimu Mafunzo ya tehama, ili waweze kupata ujuzi, pamoja nakupeleka kompyuta katika shule za serikali, ikiwa lengo nikuunganishe shule hizo na intaneti.