Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Ally Salum Hapi katika moja ya ziara zake katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo iliyopo Manispaa ya Musoma, mkoani Mara leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Ally Salum Hapi akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini katika ofisi yake na kuahidi kutoa ushirikiano unaohitajika katika kila sekta na vyombo vya usalama vilivyomo katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwenye Mkoa wake.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Ally Salum Hapi akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumannne Sagini ukarabati wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara iliyopo Manispaa ya Musoma, leo Mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Butiama leo, katika moja ya ziara yake Mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, amelitaka Jeshi la Polisi na Idara ya Uhamiaji kuendelea kushirikiana kwa pamoja ilikudhibiti moja ya changamoto iliyopo mkoani Mara ya Wahamiaji haramu. Amesema hayo leo, kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Butiama.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amekutana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, Samwel Kuboye, pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM, Mara katika ziara yake Mkoani hapo leo, amewaomba washirikiane ili kudhibiti uhalifu uliopo mkoani Mara.