MKUU wa wilaya ya Muleba Mkoani Kagera Toba Nguvilla akiwa kwenye picha mara baada ya uzinduzi wa huduma ya Meli ya Matibabu (Medical Ship) Mv.Jubilee Hope |
MKURUGENZI wa Halmahsuri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila |
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila
katika akipata maelezo kuhusu namna huduma mbalimbali zinavyotolewa
ndani ya meli hiyo
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila
akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuingia kwenye meli hiyo
NA MWANDISHI WETU,KAGERA
MKUU
wa wilaya ya Muleba Mkoani Kagera Toba Nguvilla amezindua huduma ya
Meli ya Matibabu (Medical Ship) Mv Jubilee Hope kwa wakazi wa Visiwani
hivyo ili kuweza kuondokana na changamoto ambazo walizokuwa wanakumbana
nazo wananchi awali.
Uzinduzi wa meli hiyo ya matibabu
ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Elias Mahwago
Kayandabila na viongozi wengine ambao wamefurahia uwepo wa huduma hiyo
muhimu.
Hatua hiyo inatajwa kwamba itakuwa mkombozi kwa wananchi
wa maeneo hayo yenye Kata 43 huku kata 5 za Mazinga, Ikuza, Bumbile,
Kerebe na Goziba zikiwa ndani ya Ziwa Victoria na kwa ujumla wake
inakadiriwa kuwa na wakazi takribani 68,000 kwa majibu wa sensa ya watu
na makazi ya mwaka 2012.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu
huyo wa wilaya alisema uwepo wa meli hiyo ni ukombozi wa matibabu kwa
wananchi wa maeneo hayo kutokana na awali kutokuwa na kituo cha afya
hata kimoja kwenye kata hizo jambo ambalo limepelekea halmashauri kuja
na ubunifu wa meli ya matibabu kama mkakati wa muda mfupi.
Alisema
meli hiyo Mv. Jubilee Hope inatarajiwa kuzunguka visiwa vyote 26
ambavyo vinakaliwa na watu ili kutoa huduma mbali mbali kwa wananchi wa
Muleba waishio visiwani.
Mkuu huyo wa wilaya alisema tayari
wilaya ya Muleba imeanza kutekeleza mkakati wake wa muda mrefu wa
kujenga Kituo cha Afya kwa Kila Kata iliyoko Kisiwani ambapo tayari Tsh.
Milioni 350 fedha za mapato ya ndani zimetolewa Kata ya Bumbile ili
kujenga Kituo cha Afya.
Ambapo lengo kuu lilikuwa ni kupeleka
fedha kiasi cha Milioni 500 kwa mwaka huu wa fedha wa 2021/2022 huku
uzinduzi wa meli hiyo ya matibabu ulifanywa na Mkuu huyo wa wilaya
kwenye Kisiwa cha Chakazimbwe kilichopo Kata ya Ikuza.
Mkuu huyo
wa wilaya alisema meli hiyo ya matibabu inatarajiwa kutoa huduma katika
kipindi cha miaka 5 kuanzia sasa na itatumia takribani Tsh. 1.5bilion
ambazo zimechangiwa na Serikali (Halmashauri ya Muleba), Taasisi ya Vine
Trust ya Uingereza, Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Na Kanisa la AICT
ambao wamekuwa kiungo muhimu sana katika upatikanaji wa Meli.
Kwa
kutambua umuhimu na maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka
2020 Halmashauri ya Wilaya ya Muleba imeamua kusajili Meli hiyo kama
Kituo cha Afya kwa upande wa ziwani ambapo Tsh. 119 milioni zimelipwa
MSD ili kupata uhakika wa madawa kwa wananchi.