Meneja Msimamizi wa Miradi ya Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza Tanzania {TANCDA}, Happy Nchimbi akikabidhi Tuzo ya Umahiri Uandishi wa Habari za Magonjwa Yasiyoambukiza {EAMNA 2021}, kwa mshindi Veronica Mrema wa MATUKIO NA MAISHA BLOG. Tuzo hiyo imetolewa kwa mara ya kwanza na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza Afrika Mashariki.
Meneja Msimamizi wa Miradi ya Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza Tanzania {TANCDA}, Happy Nchimbi akikabidhi cheti cha tuzo ya Umahiri Uandishi wa Habari za Magonjwa Yasiyoambukiza {EAMNA}, 2021, kwa mshindi Veronica Mrema wa MATUKIO NA MAISHA BLOG. Tuzo hiyo imetolewa kwa mara ya kwanza na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza Afrika Mashariki.
Mshindi tuzo ya Umahiri Uandishi wa Habari za Magonjwa Yasiyoambukiza {EAMNA 2021}, upande wa Tanzania Bara, Veronica Mrema wa MATUKIO NA MAISHA BLOG, akiwa ameshikilia tuzo yake {ngao pamoja na cheti}, baada ya kukabidhiwa na Meneja Msimamizi Miradi ya Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza Tanzania {TANCDA}, Happy Nchimbi.
*************************
Na Mwandishi Maalum
Wanahabari watatu wa Tanzania wameibuka kidedea katika tuzo za umahiri uandishi wa habari kuhusu afya ya uzazi, Barani Afrika za ‘Merck More Than a Mother – 2021},
Waandishi hao ni Veronica Mrema wa Matukio na Maisha Blog ambaye ameshinda katika kipengele cha vyombo vya habari mtandaoni.
Wengine ni Christina Mwakangale wa Nipashe/Guardian kipengele cha magazeti na Adam Gabriel {Hhando, wa CG FM}, kipengele cha redio.
Tuzo hiyo inaangazia masuala ya afya uzazi Barani Afrika, Shirika la Merck Foundation la Ujerumani kwa kushirikiana na Marais na Wake wa Marais Barani Afrika, limetangaza.
Zinafanyika mwaka wa nne sasa mfululizo tangu zilipoanzisha 2017/18. Hii ni mara ya tatu kwa Veronica kuwania na kutwaa tuzo hiyo, zinalenga kuhamasisha wanahabari kuelimisha jamii kuachana na mila potofu na vitendo vya unyanyapaa kwa watu waliokosa watoto {wagumba/tasa}.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Seneta Dk. Rasha Kelej, ametangaza majina ya washindi wa tuzo hiyo kupitia taarifa yake iliyotumwa kwa vyombo vya habari.
Pamoja na Watanzania hao walioshinda katika Ukanda wa Afrika Mashariki, wametangaza pia washindi wengine kutoka Ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika, Afrika Magharibi na nchi ambazo zinazungumza lugha ya Kifaransa.
Seneta Kelej ambaye pia ni Rais wa shirika hilo linaloshirikiana na marais wa barani Afrika, amesisitiza “Nina furaha kuwatangaza washindi hawa wa Merck Foundation Africa Media Recognition Awards ‘More Than a Mother’ 2021 {zaidi ya Mama}.
“Pia nachukua fursa hii kuwashukuru m
Marais wa Afrika kwa nia yao thabiti na kushirikiana nasi kama Mabalozi wa Merck Foundation.
Amevipongeza pia vyombo vya habari Barani Afrika ambavyo vimekuwa sauti ya wasio na sauti na kuongeza uelewa kwenye jamii hususan unyanyapaa kwa wagumba, tasa katika changamoto za kupata watoto.
Ameongeza “Kila mara jukumu kuu la vyombo vya habari, vina uwezo wa kuleta mabadiliko ya kitamaduni katika jamii zetu kwa njia ya gharama nafuu.
“Ninawakaribisha washindi wote kuwa wanachama wa walimu wetu wa Merck Foundation na kufanya kazi kwa karibu nasi, ili kuunga mkono, kuwawezesha wanawake na wasichana katika ngazi zote.”
“Nimefurahishwa na kazi iliyoonyeshwa na washindi wetu wote, inanipa furaha kubwa kutangaza kwamba Merck Foundation inawazawadia washindi program ya mwaka mmoja ‘MasterClass’
Amesema kozi hiyo itawajengea washindi hao uzoefu wa kipekee wa mtandaoni na kujifunza ya haraka ambayo hufikiwa popote kwa njia ya mtandao.
Ningependa kutoa wito wa kuwasilisha maombi Merck Foundation Africa Media Recognition Awards ‘Zaidi ya Mama’ kwa mwaka 2022,” ametoa rai.