Home Mchanganyiko MADARASA MAWILI YAEZULIWA, PAMOJA NA NYUMBA 36 KUTOKANA NA MVUA ILIYOAMBATANA NA...

MADARASA MAWILI YAEZULIWA, PAMOJA NA NYUMBA 36 KUTOKANA NA MVUA ILIYOAMBATANA NA UPEPO MKALI HUKO CHALINZE

0
**********************
20, January
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
MVUA iliyombatana na upepo mkali imeleta maafaa makubwa katika kata ya Lugoba halmashauri ya Chalinze  , Mkoani Pwani , baada ya kuezua  paa za madarasa mawili ya shule ya msingi  Makombe  .
Vilevile, nyumba 36 za makazi ya watu  pamoja na kuharibu mazao mbalimbali mashambani kutokana na maafa hayo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya chalinze Hassan  MwinyiKondo ,ambae aliambatana na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ramadhani Possi,  diwan wa kata Lugoba Rehema Samwel na Mwenyekiti wa huduma za jamii  Juma Mpwimbwi  walifika katika shule ya msingi Makombe kuona uharibifu uliojitokeza.
“Tumekuja hapa kujionea maafa ,”tumejionea hivyo Kubwa zaidi mikakati ya ziada ni kuhakikisha Hali ya awali inarudi , Halmashauri yetu imejipanga na tumeagiza kufanywe tathmini haraka “alisema Mwinyikondo
Diwani wa kata ya Lugoba, Rehema Mwene alieleza, Jambo hili linahitaji usimamizi wa haraka ,kwani wananchi wameshtushwa na Kama kata tumejipanga kuangalia namna ya kusaidia waliopata janga hili.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Possi anasema “Sisi Halmashauri ya Chalinze,tumetenga Milioni 300 ya kuchangia sekta ya elimu ,hili Ni suala la dharura tutalifanyia kazi baada ya tathmini kujua gharama zinazotakiwa”.
Possi alisema, hatua ya awali ni  kufanya tathimini  ya uharibifu huo ili waweze kufanya  ukarabati wa Madarasa  hayo haraka.
Mkuu wa shule hiyo,Norah Mtabwa alieleza,darasa la Saba wamehamishiwa darasa la awali wakitoka ,na darasa la pili wanapishana na darasa la kwanza na wakati kadhia hiyo ikitokea bahati nzuri ilikuwa muda wa kutoka shule.
Ofisa elimu msingi Chalinze, Mariam Kihiyo alifafanua,  madarasa yaliyoezuliwa kutokana na mvua Ni mawili ,hakuna watoto wanaokosa masomo kwakuwa wanapokezana ikiwemo wanafunzi wa Madarasa yaliyoezuliwa.