TAARIFA KWA UMMA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma mabadiliko ya tarehe ya vikao vya kitaifa vya mwezi Januari, 2022 kama ifuatavyo:-
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitafanyika tarehe 20 Januari, 2022 badala ya tarehe 18 Januari, 2022 katika ofisi za Makao Makuu (White House), Dodoma.
Kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Maandalizi ya vikao vyote hivyo yamekamilika.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
SHAKA HAMDU SHAKA
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA ITIKADI NA UENEZI.