RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Afisa wa Polisi Sami Humaid alipotembelea Kituo cha Polisi “Smart Police Station “ katika viwanja vya maonesho ya Dubai Expo 2020, chenye kutoa huduma kupitia njia ya mtandao.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Afisa wa Polisi wa Kituo cha Polisi kinachotowa huduma kwa Wananchi kupitia njia ya mtandao “Smart Police Station” Sami Humaid (kulia kwa Rais) akitowa maelezo yamashine inayotumika kuwasilisha malalalamiko ya Wananchi, wakati alipotembelea maonesho ya Dubai Expo 2020.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja wa Maofisa wa Polisi wa Kituo cha “Smart Police Station” baada ya kutembelea Kituo hicho kinachotowa huduma zake kupokea malalamiko ya Wananchi kupitia kifaa maalum kwa njia ya mtandaoa na (kulia kwa Rais) Balozi wa Tanzania U.A.E Balozi Mohammed Abdalla Mtinga na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Kituo hicho na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, wakiwa na Maofisa wa Polisi wa “Smart Police Station”.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzin Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya kifaa maalum kinachotumika katika kuwasilisha kesi kupitia njia ya mtandao.”Smart Police Station” kutoka kwa Afisa wa Polisi Sami Humaid, wakati akitembelea maonesho ya Dubai Expo 2020.(Picha na Ikulu)
….…………………………..
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi tarehe 17 Januari, 2022 ametembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya EXPO 2020 Dubai yanayoendelea katika Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE)
Rais Mwinyi ambaye yupo katika ziara ya Kiserikali nchini humo ametembelea banda la Tanzania katika Maonesho ya Expo Dubai2020 kwa ajili ya kujionea jinsi Tanzania inavyotumia fursa ya Maonesho hayo ya Makubwa Duniani kutangaza Biashara na Uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na Uchumi wa Bluu, Utalii, Madini, Nishati na Kilimo.
Mhe. Rais Mwinyi amepongeza ushiriki wa Tanzania kwenye Maonesho hayo ikiwa ni miongoni mwa Nchi 192 zinazoshiriki katika Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 1 Oktoba , 2021 na yanatarajiwa kukamilika tarehe 31 Machi, 2022 ambapo, Ushiriki wa Tanzania kwenye Maonesho hayo unaratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Pia Mhe. Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi ametembelea Kituo cha Polisi cha mtandao “ Smart Police Station “ kwenye Maonesho hayo ambapo alipewa maelezo kuhusu kifaa maalum kinachotumika kuwasilisha kesi kwa njia ya mtandao.
Katika ziara hiyo, Rais Dk. Mwinyi amefuatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi pamoja na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.