Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo aKIkagua ujenzi wa jengo la Wizara hiyo unaoendelea katika eneo la Mtumba jijini Dodoma. Wakati wa ukaguzi huo Katibu Mkuu huyo amepongeza juhudi na kasi ya ujenzi na kumtaka Mkandarasi ambaye ni SUMA JKT kuhakikisha inakamilika kwa wakati huku akiwataka TBA ambao ni Mshauri Mwelekezi kuhakikisha kazi inafanyika kwa kuzingatia viwango na ubora unaohitajika.