Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Balozi Mha. Aisha Amour, akipokea nyaraka za ofisi hiyo kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Sekta hiyo Mha. Joseph Malongo, wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi iliyofanyika leo katika ofisi za wizara hiyo zilizopo mji wa Serikali Mtumba.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Balozi Mha. Aisha Amour, akielezea jambo mara baada ya makabidhiano ya ofisi, kati yake na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi , Mhandisi Joseph Malongo (aliyeketi Kushoto), yaliyofanyika leo katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba.
Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, (Sekta ya Ujenzi), wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Mha. Aisha Amour (hayupo pichani), wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi, yaliyofanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba.