Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa kikao baina ya uongozi wa mkoa na watendaji wa kata, mitaa na maafisa afya kutoka maeneo yote ya jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri,,akizungumza wakati wa kikao baina ya uongozi wa mkoa na watendaji wa kata, mitaa na maafisa afya kutoka maeneo yote ya jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru,akiwaeleza watendaji kuzingatia suala la usafi katika jiji hilo wakati wa kikao baina ya uongozi wa mkoa na watendaji wa kata, mitaa na maafisa afya kutoka maeneo yote ya jijini Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk. Fatuma Mganga,akizungumza wakati wa kikao baina ya uongozi wa mkoa na watendaji wa kata, mitaa na maafisa afya kutoka maeneo yote ya jijini Dodoma.
Mkuu wa Idara ya mazingira jiji la Dodoma Dickson kimaro,akieleza mipango ya jiji hilo kuhusu usafi wakati wa kikao baina ya uongozi wa mkoa na watendaji wa kata, mitaa na maafisa afya kutoka maeneo yote ya jijini Dodoma.
Afisa Mtendaji Kata ya Uhuru Christina Mpete,akichangia mada wakati wa kikao baina ya uongozi wa mkoa na watendaji wa kata, mitaa na maafisa afya kutoka maeneo yote ya jijini Dodoma.
Mtendaji Kata ya Viwandani Emanuel Nyenje akichangia hoja wakati wa kikao baina ya uongozi wa mkoa na watendaji wa kata, mitaa na maafisa afya kutoka maeneo yote ya jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatili Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka (hayupo pichani),wakati wa kikao baina ya uongozi wa mkoa na watendaji wa kata, mitaa na maafisa afya kutoka maeneo yote ya jijini Dodoma.
……………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
JIJI la Dodoma kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa limeanza kutekeleza agizo la Makamu wa Rais, Dk.Philip Mpango huku Mkuu wa Mkoa Anthony Mtaka akishauri kuhuwishwa kwa sheria ya usafi ya jiji ili kuwe na usafi endelevu.
Dk. Mpango alitoa wiki mbili kuhakikisha takataka zote zinaoendolewa na kuweka mikakati ya kuhakikisha Jiji la Dodoma lionekane safi katika kata na mitaa yote.
Akizungumza wakati wa kikao baina ya uongozi wa mkoa na watendaji wa kata, mitaa na maafisa afya kutoka maeneo yote ya jijini Dodoma, Mtaka amesema suala la usafi linatakiwa kuwa endelevu.
“Tuone namna ya kuhuisha sheria ya Jiji kuhusu masuala ya usafi, hata ikipidi zile faini mtu atakaye kamata anayetupa taka basi apewe kamisheni na zingine zitumike kuimarisha usafi”amesema
Pia, amewataka watendaji wahakikishe kila eneo la biashara wafanyabiashara waweke vyombo vya taka ili kudhibiti uzagaaji na utupaji taka ovyo na kusisitiza suala la suala la kuzagaa kwa taka linakuwa historia.
Aidha, Mtaka amemtaka Mkurugenzi wa jiji hilo kuwa mkali kwa watendaji ambao wanafanya kazi kwa mazoea na vituo vya kazi watendaji wa Kata na Mitaa ambao utendaji kazi wao umekuwa sio mzuri huku akisisitiza kutoa kipaumbele kwa wale ambao ni watendaji wabunifu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru amewataka watendaji, maafisa afya na mazingira kufuata sheria za mazingira kwa kutoa faini kama kunamtu anastahili adhabu hiyo.
” Kuanzia sasa mimi na timu yangu tutanza kutembea mtaa kwa mtaa kata kwa kata, nyumba kwa nyumba ili kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa maagizo, ni sisitize hii hali iliyojitokeza haita jirudia na sitavumilia.”amesema
Aidha, Mafuru alimuagiza afisa utumishi kuwaandikia barua watendaji wa mtaa na kata ambao wamekaidi kikao alichoitisha cha kuweka mikakati ya kutekeleza agizo la Makamu wa Rais.
Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma Dk. Fatma Mganga amewataka Maafisa Mazingira,Maafisa Afya na watendaji wote kuwaonyesha wananchi kufanya usafi kwa vitendo.
“Kuna jumla ya watendaji 239 walioajiliwa serikalini sasa kunasababu gani ya jiji lionekane chafu…hapa kunamahali hatuwajibiki ipasavyo na tumejisahau lazima tujiulize tumefika hapa mpaka viongozi wa juu wanakuja kutukosoa sisi wachafu kwa sababu gani,” amesema.