Wadau wa Afya
wamekutana jijini Dar Es Salaam kufanya tathmini na kuweka mikakati ya
kuimarisha matumizi sahihi ya vituo vilivyoanzishwa kutoa mafunzo kwa wataalamu
wa Sekta ya Afya kwa njia ya mtandao (Project – ECHO), pamoja na kuendelea
kufunga vifaa katika vituo vipya vitakavyofunguliwa hivi karibuni katika Wilaya
chache zilizosalia kupata huduma hiyo.
Mpaka sasa tayari vituo
265 vimeshaanzishwa nchi nzima na mikakati inaendelea ya kuongeza vituo zaidi
mikoa ya Kusini na Magharibi.Kikao hicho cha wadau kimefadhiliwa na Serikali ya Marekeni kupitia mradi wa CDC unaotekelezwa na
Chuo Kikuu Mzumbe.Mratibu wa Mradi wa ECHO kitaifa (Project ECHO), Bw. Jacob Lusekelo akiwasilisha ripoti ya tathmini wakati wa kikao cha wadau walipokusanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Dr. Idda Lyatonga, mmoja
wa wataalamu wa tathimini na mratibu wa mpango wa mafunzo kwa njia ya Mtandao
(Project Echo) akichangia jambo kwenye kikao cha wadau walipokutana Hoteli Sea
Scape hivi karibuni.Mtaalamu wa Maabara kutoka TAMISEMI Bw. Alouis Nicas, akichangia jambo kuhusu mafanikio ya mradi huo kwa wataalamu wa afya waliopo Wilayani baada ya vituo kadhaa kufunguliwa na kuanza kutoka huduma.