KLABU ya Yanga, leo Jumapili imepanga baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union, kumtambulisha nyota wake wa kimataifa ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wao.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, umepangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa kuanzia saa 10:00 jioni.
Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa Yanga, Haji Manara, alisema mchezaji huyo walimuwinda kwa
muda mrefu na usajili walioufanya hawajakosea.
wetu rasmi mara baada ya kumaliza mchezo na Coastal hapohapo uwanjani tutamtangaza mchezaji wetu mpya wa kimataifa ambaye tayari kila kitu kimeshakamilika, imebakia tu kumtambulisha kwa wapenzi na mashabiki wetu,” alisema Manara Kuelekea mchezo huo dhidi ya Coastal Union, Manara alisema wanawaheshimu wenyeji
wao wakiangalia na matokeo ya misimu kadhaa nyuma waliyopoteza uwanjani hapo, hivyo wamekuja kwa tahadhari zote wakitambua utakuwa na “Tunafunga usajili ushindani mkali.
“Mechi sio ya kawaida kwetu, tumeipa uzito mkubwa, Yanga inawaheshimu Coastal, lazima tuwaheshimu kwa vyovyote vile. Hatuwezi kuja Tanga kwa kuwadharau, ili ushinde ubingwa lazima ushinde mechi ngumu kama hizi za nje.
“Baada ya kupoteza Kombe la Mapinduzi, nia, malengo na dhumuni la klabu wachezaji wetu wanajua hatuna chochote cha kupoteza, hivyo tunakwenda kuhakikisha tunapata alama tatu muhimu dhidi ya Coastal Union,” alimaliza Manara.
STORI: DENIS CHAMBI, TANGA