Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui (kushoto) akipokea msaada wa vifaa Tiba vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 114,521.27 kutoka kwa Taasisi ya Helping hand ya Marekani wakishirikiana na Taasisi ya Muzdalifa iliyopo Zanzibar ,huko Wizarani Kwake Mnazimmoja Zanzibar (kulia) ni mshauri msaidizi wa taasisi hiyo Irfan Khurshid.
Mshauri msaidizi Taasisi ya Helping Hand ya Marekani Irfan Khurshid akizungumza katika makabidhiano ya vifaa Tiba baina Yao na Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto hafla iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mnazmmoja Zanzibar.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee , Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui akitoa neno la shukurani mara baada ya kupokea msaada wa vifaa Tiba vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 114,521.72 kutoka kwa Taasisi ya Helping Hand huko Wizarani kwake Mnazimmoja Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR.
*******************************
Na Issa Mzee – Maelezo 14/01/2022.
Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui amekabidhiwa masaada wa Vifaa tiba kutoka Taasisi ya Helping Hand kutoka Marekani wenye thamani ya Dola za kimarekani 114,521.72.
Makabaidhiano hayo yalifanyika Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar, baina ya Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto na Taasisi ya Helping Hand ya Marekani kwa kushirikiana na Taasisi ya Muzdalifa iliyopo Zanzibar.
Mapema Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui amesema msaada huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii.
Alisema kuwa, lengo la msaada huo ni kuwasaidia wananchi, hivyo aliihakikishia taasisi hiyo kuwa vifaa hivyo vinatumika ipasavyo na kuwafikia walengwa waliokusudiwa.
Aidha aliahidi kuendeleza ushirikiano wa karibu baina ya Wizara ya afya na Taasisi hiyo ili lengo la kuboresha sekta ya afya liweze kufikiwa nchini.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mshauri Msaidizi wa taasisi ya Helping Hand, Irfan Khurshid alisema msaada huo wa vifaa tiba ni miongoni mwa jitihada za kuisaidia sekta ya afya Zanzibar iweze kutoa huduma bora kwa jamii.
Alieleza kuwa taasisi hiyo ina mpango wa kuendelea kutoa misaada mbalimbali ya sekta ya afya kuja Zanzibar, ili wananchi wa Unguja na Pemba waweze kunufaika.