*******************
Abel Ngapemba na mkewe Anna Walikua mfano mzuri sana hata kwetu tuliowatangulia.
Jambo la kutufariji sisi ndugu jamaa na marafiki wa Abel ni huyu kijana Albert Abel Ngapemba.
Kijana huyu toka awasili Dar na wenzake wa UDOM ambako ndiko anasoma, amekua kiongozi mzuri wa familia na aliyekua akisaidia kupanga mipango, ratiba na hata kuwanasihi wafiwa akiwemo mama yake Anna na bibi yake (Mama Abel).
Kwa maneno ya busara alikua amewafanya Anna na Mama Abel kuwa na nguvu na kuupokea msiba kwa ujasiri.
Ni Albert aliyewasemesha wafiwa kwa ushupavu na wakamsikia.
Katika ibaada ya mazishi ya Abel iliyofanyika katika
Kanisa Katoliki, Kanisa Kuu la Mtatakatifu Andrea Mtume Parokia ya Ifakara,kijana huyu ametajwa kama mtu anayewakilisha u-Abel kwetu sote sisi wafiwa.
Yako mengi tunayojifunza kwenye familia ya mwenzetu Abel.
Jambo lingine la kiimani ni kwamba wakati mwili wake unahifadhiwa kwenye makaburi ya familia hapo Ifakara,ilinyesha mvua kidogo ya ghafla,iliyotafsiriwa kama ni salam za kumuaga huku radi ikinguruma mithili ya mizinga ipigwayo kwa askari mwenye cheo cha juu anapozikwa.
Binafsi nilifarijika na kuamini kwamba kwa Mungu ndugu yetu Abel atakua amepokelewa kishujaa na saluti kutokana na nyendo na wema wake duniani kwetu sote na familia yake.
Akiongea wakati wa salamu mbalimbali, Zamaradi Kawawa aliyemwakilisha Msemaji Mkuu wa Serikali alisema Abel kila alipopita alifanya kazi kwa weledi, uadilifu na kujituma.
Alisema Abel alikuwa ni Mseminari wa kweli kwa matendo na imani.
Mungu amempenda zaidi yetu na ametupa ishara njema kwake. Tumejifunza.
Ahsante Mungu.
Ni Mimi Mbaraka Islam