WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Elimu OR-TAMISEMI, Gerald Mweli ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Katibu wa TSC Bi.Paulina Nkwama,akielezea malengo ya mkutano wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Muwakilishi wa Kamishna wa Elimu Bw.Venance Manoni,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Alhaji Abdul Maulid akitoa neno la shukrani kwa niba ya washiriki kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa (hayupo pichani) mara baada ya kuzindua kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa,akizindua kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda.Wengine Pichani ni Katibu Mkuu TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe (wa pili Kulia),Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Elimu OR-TAMISEMI, Gerald Mweli (Kushoto).Muwakilishi wa Kamishna wa Elimu Venance Manoni (wa Kwanza Kulia) hafla ya uzinduzi huo umefanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa akisoma maandishi baada ya kuzindua kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa akiwa katika picha mbalimbali za pamoja na washiriki mara baada ya kuzindua kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
……………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa ametoa maelekezo saba kwa viongozi wa Mikoa na Halmashauri ikiwemo kuhakikisha hakuna mwanafunzi wa elimu ya awali, darasa la kwanza au kidato cha kwanza anayetozwa mchango wowote kama sharti la mwanafunzi kuandikishwa.
Maagizo hayo ameyatoa leo Januari 14,2022 Jijini Dodoma wakati akifungua Mafunzo kwa Maafisa Elimu Mikoa, Maafisa Taaluma Mikoa na wathibiti ubora wa shule kanda pamoja na kuzindua kalenda za utekelezaji wa Mitaala ya elimu ya Awali,Msingi na Sekondari.
Waziri Bashungwa amesema wakati shule za msingi na sekondari zinatarajiwa kufunguliwa tarehe 17 Januari, 2022, kumeanza kutokea malalamiko toka kwa wananchi, kuhusu kutozwa michango mbalimbali, bila kufuata utaratibu.
“Wanafunzi kupelekwa kuandikishwa shule, na kisha kuambiwa shule zimejaa, au wazazi kuwapeleka shule wanafunzi, na kukuta shule haina mwalimu anayetakiwa kuwandikisha shule, kwa maana wanakuta shule zimefungwa,”amesema.
Amesema changamoto hizi, zimekuwa zikileta usumbufu kwa wazazi na wanafunzi pamoja na kuleta usumbufu usio wa lazima kwa wananchi.
Amesema vikwazo na kero hizi zimefifisha kwa kiasi kikubwa, uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza na elimu ya awali.
Kutokana na hali hiyo Waziri Bashungwa amewaelekeza viongozi wa Mikoa, Halmashauri na Shule, kuhakikisha hakuna mwanafunzi wa elimu ya awali, darasa la kwanza au kidato cha kwanza anayetozwa mchango wowote kama sharti la mwanafunzi kuandikishwa.
Pia,kila shule kuwepo na mwalimu mmoja kwa ajili a kuandikisha watoto katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wapo likizo.
“Viongozi wote wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa Mwongozo wa utoaji wa Elimumsingi Bila Malipo. Mheshimiwa Rais ameongeza fedha zinazotolewa kila mwezi, kwa ajili ya kugharimia elimu bila malipo, kutoka shilingi bilioni 23 kwa mwezi hadi kufikia bilioni 26 kwa mwezi,”amesema.
Pia amewaelekeza Maafisa elimu wa kata kwa kushirikiana na watendaji wa kata,mitaa na vijiji, wabainishe watoto wote wanaotakiwa kuandikishwa shule na wawasisitize wazazi/walezi kufanya hivyo.
“Viongozi wote wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuendelea kufafanua utekelezaji wa Waraka wa Elimumsingi Bila Malipo kwa wazazi, jamii na wanafunzi,”amesema.
Pia,kila kundi litimize wajibu wake ili watoto wote waandikishwe, na kuendelea na masomo, katika ngazi husika.
“Kufanya zoezi la utambuzi wa watoto wenye mahitaji maalum ni suala endelevu hapa nchini. Mwaka 2018 na 2021 Ofisi ya Rais – TAMISEMI ilifanya ubainishaji wa watoto hao, nakuwaandikisha shule,”amesema.
Waziri Bashungwa pia ameelekeza Mikoa yote iimarishe na kutumia vituo vya Uchunguzi Education Service Resource Assessment Centre (ESRAC) ili visaidie katika kubainisha wanafunzi wenye mahitaji maalum, na kushauri wapelekwe katika shule maalumu, vitengo vya elimu maalum au shule jumuishi.
Kuhusiana na kalenda,Waziri Bashungwa amesema kusudi la kuandaa kalenda ni kuhakikisha kuwa, kunakuwepo na ulinganifu na usawa, wa ukamilishaji katika utekelezaji wa mitaala wa ngazi husika, katika maeneo yote ya nchini.
“Kalenda hii ni ya kwanza kuandaliwa na Serikali. Kalenda hii itawezesha wasimamizi wa elimu kufanya usimamizi, ufuatiliaji, na tathmini ya utekelezaji wa mitaala kwa urahisi,”amesema
Vilevile, kalenda hiyo itawapa fursa wanafunzi wanaohama kutoka shule moja kwenda nyingine kuwa na mwendelezo wa aina moja wa mada zinazofundishwa.
Waziri Bashungwa amewaagiza Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya, kuwasimamia Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu wa Masomo, kuzingatia kalenda ya utekelezaji wa mtaala, ili wawe na ufundishaji na ujifunzaji wenye tija na mahiri, badala ya kuwekamsisitizo katika ukaririshaji wa mada.
“Hivyo, natumia fursa hii kuwaagiza Maafisa Elimu Mikoa, kutoa mafunzo ya matumizi ya Kalenda ya Utekelezaji, katika Halmashauri zenu zote, kabla au ifikapo tarehe 1 Februari, 2022,”amesema.