Meneja Ufundi wa Mamlaka ya MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Mhandisi Rashid Shabani akieleza jambo wakati wa semina hiyo
AFISA Uhusiano wa MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Devotha Mayalla akizungumza wakati wa semina hiyo
Meza Kuu wakiwa kwenye semina hiyo
Mmoja wa washiriki wa Semina hiyo akiuliza swali
Sehemu ya Washiriki katika Semina hiyo wakifuatilia mawasilisho mbalimbali
Sehemu ya Washiriki katika Semina hiyo wakifuatilia mawasilisho mbalimbali
Sehemu ya Washiriki katika Semina hiyo wakifuatilia mawasilisho mbalimbali
********************
OSCAR ASSENGA, TANGA.
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) imesema kwamba wataanzisha operesheni ya kuzuia mivujo ya maji nyuma kwa nyuma ili kuweza kuondokana na upotevu wa maji yanayopotea kutokana na uwepo wa hali hiyo.
Hayo yalisemwa leo na Meneja Ufundi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani wakati akiwasilisha wasilisho kuhusu kujenga uelewa kuhusu udhibiti wa maji yanayopotea.
Wasilisho hilo aliliwasilisha katika semina kwa wateja wa Jiji la Tanga kuhusu kuanza kwa utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa mteja.
Licha ya hivyo pia waliitumia kuwajengea uelewa kudhibiti maji safi yanayopotea iliyofanyika Ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo eneo la Mwakidila Jijini Tanga.
Alisema operesheni hiyo itakuwa ni mwarobaini wa kuhakikisha maji yanayopotea yanadhibitiwa na hatimaye kuondokana na tatizo hilo ambalo wakati mwengine limekuwa likiwasababishia hasara.
“Tutaanzisha operesheni zuaia mivujo ya maji nyumba kwa nyuma kwqa kuangalia mazingira na hilo litatusaidia kuweza kupunguza tatizo la upotevu wa maji”Alisema
Hata hivyo alisema pia wataunda kikosi kazi cha kufuatilia wezi wa maji majumbani ambao wamekuwa wakishirikiana na wafanyakazi wao ambao sio waaminifu.
Awali akizungumza wakati akifungua semina hiyo Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema wanapenda wananchi waelewe njia mbalimbali ambazo maji yanapotea na namna gani kama viongozi, wananchi wanaweza kusaidia kuokoa maji yanayopotea ili huduma ziweze kuwa endelevu.
Alisema suala la pili kuna mkataba wa huduma kwa mteja ambapo mwaka jana walikutana na baadhi yao kujadiliana suala hilo ambapo alisema kwa sasa mkataba huo umepatikana na wanapaswa kuelewa mkataba huo.
Alisema kwani viongozi ni watu wa kwanza kuweza kupata fursa ya kupata uelewa na mkataba huo .