***********************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Mwanafunzi wa shahada ya uhasibu katika chuo cha uhasibu Arusha(IAA),Juma Masende ameweka nia ya kuwania nafasi ya spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na kuwa ana uwezo kutokana na nafasi mbalimbali za uongozi ambazo amewahi kuongoza akiwa chuoni .
Akizungumza na waandishi wa habari ,Masende amesema kuwa, lazima achukue fomu ya kuwania nafasi hiyo ili aweze kusaidia serikali katika kusimamia rasilimali za nchi pamoja na matumizi bora ya rasilimali.
“Mimi nataka kugombea hii nafasi kwani mimi ni kijana mdogo ambaye Nina uchungu na nchi yangu na nataka kusimamia rasilimali za nchi yetu kikamilifu na kuhakikisha zinawanufaisha wananchi wake kwani uwezo wa kusimamia rasilimali ninao kutokana na uzoefu nilio nao kwa muda mrefu Sasa.”amesema Masende.
Amesema kuwa, watawakaribisha wawekezaji nchini na watatafuta misingi tuliojiwekea huku tukisimamia kanuni na sheria za nchi kikamilifu kwani ndio mwongozo wetu.
Amesema atasimimia kanuni ili kila Mtanzania aweze kunufaika na rasilimali za nchi pasipokuwepo upendeleo wowote kwani kiongozi anatakiwa kuwa muwazi na mzalendo ambapo wanategemea kupambania rasilimali ziliopo nchini kwa maslahi ya nchi.
“Mimi ninachojua ni kuwa nchi yetu hii ni tajiri sana kwa sababu tuna rasilimali nyingi ambazo tukizisimamia kupitia kanuni zetu kwa mwenendo mzuri pasipo kuvunja sheria kila Mtanzania mmoja mmoja atanufaika na rasilimali zilizopo kwani Tanzania tumejaliwa neema ya kutosha ambayo tukipata viongozi wazuri wenye kufuata maadili tutaweza kufika mbali Sana”amesema Masende.
Masende amesema vijana ndio nguzo ya Taifa na wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii wakimuunga mkono Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha tunayaunga mkono na kuyaendeleza yale yote anayoyafanya kwa mustakabathi wa nchi yetu.
Aidha Masende aliwaomba watanzania kumuunga mkono na kumwombea aweze kupata nafasi hiyo ya uspika kwani anataka kuwa kiongozi wa kuigwa na jamii na hata vijana wenzake ilo waweze kutambua kuwa swala la kuwania uongozi ni la kila mmoja bila kujali umri kikubwa ni uwe na uwezo wa kuongoza nchi tu.