Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda, akikabidhiwa nyaraka kama ishara ya kukabidhiwa rasmi ofisi ya Wizara hiyo na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Prof. Joyce Ndalichako ambaye kwa sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu tukio hilo limefanyika leo Januari 13,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akionyesha nyaraka mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi ya Wizara hiyo na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Prof. Joyce Ndalichako ambaye kwa sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu tukio hilo limefanyika leo Januari 13,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza baada ya kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Prof. Joyce Ndalichako ambaye kwa sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu tukio hilo limefanyika leo Januari 13,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akisisitiza jambo kwa watumishi wake baada ya kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Prof. Joyce Ndalichako ambaye kwa sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu tukio hilo limefanyika leo Januari 13,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako,akizungumza na viongozi wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia wakati wa makabidhiano ya Ofisi leo Januari 13,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akizungumza wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya wizara hiyo kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Prof. Joyce Ndalichako ambaye kwa sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu tukio hilo limefanyika leo Januari 13,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiana rasmi ofisi ya Wizara hiyo tukio hilo limefanyika leo Januari 13,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda, akiagana na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Prof. Joyce Ndalichako ambaye kwa sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu baada ya makabidhiano ya Ofisi tukio hilo limefanyika leo Januari 13,2022 jijini Dodoma.
………………………………………………
Na Alex Sonna, Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda, amesema Wizara itashirikisha wataalam wa masuala ya elimu nchini ikiwamo Wastaafu katika uboreshaji wa elimu.
Hayo ameyasema hayo leo Januari 13,2022 jijini Dodoma wakati wa hafla ya makabidhiano kati yake na aliyekuwa Waziri Wizara hiyo, Prof.Joyce Ndalichako ambaye amehamishiwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu
Amesema kuna kazi kwasasa inaendelea ndani ya Wizara hiyo ya mapitio ya mitaala na jamii itakuwa inajulishwa kinachoendelea huku akisema milango ya Wizara ipo wazi kwa wataalam hao kutoa maoni yao yatakayosaidia kuwa na elimu bora.
“Prof.Ndalichako amesema kuna wakati walikuwa hawalali kweli, maana unajadili suala la elimu ya nchi yetu, na kama tutahitaji input za wataalam kutoka nje ya Wizara, tuna wataalam wengi mno huko na wengine wamestaafu tutawaita tuzungumze ili tukitoka tuwe na kitu kimoja,”amesema.
Amesema kuna mambo mengi yanahitaji kujadiliwa na wasiwe waoga kuleta wataalam wa ndani ya Nchi kutoka mahali popote.
“Kwa mfano kuna suala kuwa elimu yetu inatoa watu ambao hawaajiriki hili ni suala ambalo lazima tujadili humu ndani, lakini michakato imeshaanza, na majadiliano yataendelea na najua maoni yanakusanywa kwa watu na najua jinsi gani hawaajiriki inawezekana pia uchumi unachangia,”amesema.
Amesisitiza kufanya kazi kwa bidii bila woga na kuhimiza kufanya kazi kwa ushirikiano.
“Mkiniona naenda mahali sio nyie ndo wataalamu niambieni sio mnaanza kusema Waziri tunamuona anachanja mbuga kwingine tumuone atafika wapi, naomba tuzungumze mambo humu ndani tushauriane na kuwa na uamuzi wa Wizara,”amesema.
Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, amesema kuhudumu kwa muda mrefu kwenye Wizara hiyo kumetokana na ushirikiano alioupata kutoka kwa watendaji wake.
“Naomba mtoe ushirikiano zaidi kwa Prof.Mkenda, mimi Mwalimu, yeye ni mchumi naamini ataleta vitu vyenye tija zaidi ana uwezo mkubwa,”amesema.
Amebainisha kuwa kuna kazi mbalimbali zinaendelea ikiwamo utayarishaji wa miongozo ya shule shikizi.
“Tumefanya kazi vizuri nawashukuru sana na tuendelee kushirikiana katika majukumu yangu mapya, katika kukuza ujuzi, ajira na watu wenye ulemavu, tutaendelea kukutana, ili kuwaandaa watanzania kuwa na sifa zinazokubalika eneo la ajira,”amesema.